The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Poleni Wamachinga

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amewapa pole wamachinga kufuatia kuteketea kwa soko lao la Karume ambapo walikuwa wakifanya biashara zao na kujiingizia kipato.

 

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne, Januari 25, 2022, wakati akizungumza na viongozi wa wamachinga Ikulu Dar es Salaam na kuongeza kuwa Serikali inawatambua rasmi Machinga kama kundi maalum, na litakuwa moja ya Makundi yatakayohudumiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalum.

 

“Moto huu una sababu kadhaa, Kariakoo tuliambiwa hitilafu ya umeme, Karume ripoti ya awali tunaambiwa mishumaa lakini hata moto unapoendelea magari yakiwa yanakuja hayana maeneo ya kupita na kwenda kuzima moto, tujipange ili magari yaweze kupita kwa urahisi, wale wanaopika kuna ile ‘nabandika maharage kesho nikija nitakuta yameiva’ inawezekana kabisa moto ukashika kitu moto ukaendelea.

 

“Lingine ni suala la Bima kuna wale ambao labda amekata Bima ya biashara yake lakini kwa miaka kadhaa hajafaidi matunda ya Bima yake kwahiyo anaamua tu ‘ngoja niweke kicheche cha moto hapa kukiungua Mimi kwasabau nina Bima nitalipwa na Bima’ hilo nalo lipo.

 

“Jingine ni hawa wanaochukua mizigo madukani inawezekana Mtu kachukua mzigo mkubwa kauza, moyo wa ushetani unamtuma asiende kurudisha, weka moto mwenye duka atajua soko limeungua au karume imeungua kwahiyo sina cha kulipa na huenda mwenye duka ana bima atalipwa huko, ndio maana nimesema tumekua sasa tujisimamie,” amesema Rais Samia.

Leave A Reply