The House of Favourite Newspapers

Askofu Adaiwa Kupotea Katika Mazingira ya Kutatanisha

0

Mke wa Askofu Mulilege Kameka marufu Mzee wa Yesu, Greena Mkoma alipokuwa akizungumza na wanahabari (hawapo pichani ).

 

 

ASKOFU wa Kanisa la House of Player Shield of Faith Christian Christian Fellowship Church lililopo Boko Magengeni Dar, aitwae Mulilege Kameka maarufu kama Mzee wa Yesu anasakwa na waumini pamoja na familia yake baada ya kutoweka katika mazingira yaliyodaiwa kuwa na utata.

Mmoja wa viongozi wa kanisa hilo Nazar Nicolas naye akisisitiza jambo kuhusiana na taarifa hizo.

 

 

Akizungumza na wanahabari kanisani hapo mke wa mchungaji huyo, Greena Mkombo amesema wiki iliyopita wakiwa nyumbani wanapoishi hapo Boko walikuja watu wasiofahamika na magari kadhaa na kujitambulisha kuwa wanatoka idara za usalama na kumchukua mumewe huyo na kutoweka nae.

Baada ya mumewe huyo kutoweka mke wa askofu huyo na waumini wa kanisa hilo walianza kumfuatilia askofu huyo kwenye idara mbalimbali za usalama bila mafanikio.

Sehemu ya waumini wa kanisa hilo.

 

 

“Nilikwenda idara mbalimbali kumsaka mume wangu nikiwa na waumini lakini kila tulipofika walituambia kuwa hayupo hivyo mpaka sasa bado hatujajua alipo.

 

“Kama anashikiliwa na chombo chochote tungeambiwa ili japo tumpelekee hata mahitaji muhimu ikiwemo chakula maana kutokana na afya yake maana alishauriwa na daktari kutumia vyakula maalum”. Alisema mke wa askofu.

 

Naye mmoja wa viongozi wa kanisa hilo aliyejitambulisha kwa jina la Nazar Nicolas naye alielezea jinsi walivyoangaika kumsaka askofu wao huyo.

 

Kufuatia sakata hilo mwanabari wetu alizungumza na Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Kamishna Msaidizi (ACP) Ramadhani Kingai ambaye alisema anachojua askofu huyo anashikiliwa na askari wa uhamiaji ambao wanachunguza suala la uraia wake na si kupotea wala kutekwa kama wanavyodai waumini hao.  Waache kuzungumza vitu ambavyo si vya kweli alisisitiza kamanda Kingai.                                                                                                                                                                    HABARI/PICHA NA ISSA MNALLY /GPL

Leave A Reply