The House of Favourite Newspapers

Askofu Chengula: Ujumbe wa Maaskofu Unalenga Wanafiki Wanaojidai Wakristo

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya, Evarist Chengula amefungukia kuhusu ujumbe uliotolewa hivi karibuni na maaskofu huku akiwataka Watanzinia kuelewa kwamba maaskofu hawana nia mbaya bali wanachotaka ni kila mtu ashiriki katika kulitakia taifa upendo wa kweli.

Ameeleza ujumbe wa maaskofu unawalenga wanafiki ambao wanajidai kuwa Wakristo lakini hawana misimamo ya Kikristo na kuwataka waumini wa Kanisa hilo nchini  kuchagua viongozi sahihi na watakaokidhi mahitaji yao badala ya kufanya makosa kwa kuchagua viongozi wasiofaa na kuanza kulalamika baada ya uchaguzi.

 

TAZAMA VIDEO YA IBADA

 

Chengula ametoa ujumbe huo katika mahubiri aliyotoa kwenye Ibada ya Ijumaa Kuu inayofanyika katika Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Parokia ya Mtakifu Francisco wa Asizi, Mwanjelwa mkoani Mbeya.

Amesema imekuwa ni kawaida kwa maaskofu na wadau wengine kuanza kukosoa viongozi baada ya uchaguzi, jambo ambalo halina faida sana, na hivyo wao kama maaskofu mwaka huu wameamua kuwataka waumini wao kuwapima kwa umakini watu wote watakaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo kwa kuanzia na uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwakani.

 

“Ni vita yetu sote, tukipata viongozi wabaya tunaumia wote, tukipata viongozi wazuri tutafurahi wote, kila mmoja aone kiu ya Tanzania hii kuwa nchi ya upendo,” amesema Askofu huyo.

Amesema wanachokifanya viongozi wa dini si kuwaelekeza waumini wao chama cha kuchagua, bali kuwapima wagombea kabla ya kuwachagua kwani endapo chama kitaweka mgombea asiyefaa, waumini watalazimika kumchagua hata kama hafai.

Comments are closed.