The House of Favourite Newspapers

WADAU WATARAJIA KITU TOFAUTI KUTOKA TECNO

KAMPUNI ya simu ya TECNO kufuatia ongezeko la matumizi ya simu za mkononi, makampuni mbalimbali yamekua yakija na matoleo tofauti lakini kampuni ya Tecno ndiyo ya kipekee  kufanya vyema sokoni, kampuni hiyo  imekuwa ndiyo kampuni pendwa zaidi katika kuzalisha kile kinachomstahili mteja.

Tayari pameshakua na minong’ono ya hapa na pale baina ya wadau wa simu janja “smart phone” ikiinyooshea vidole kampuni ya TECNO, kwa kuihusisha kampuni hiyo na ujio wa toleo jipya ambayo ni muendelezo wa Camon.

 

Mbali na picha mbalimbali zilizozagaa mtandaoni zikionesha muonekano tofauti wa simu hiyo mpya kuzinduliwa, tayari kurasa za mitandaoni zimezua mijadala inayokosa majibu sahihi kuhusiana na simu hiyo, baadhi wakiifananisha simu hiyo mpya kutoka TECNO na zile za kampuni ya Samsung na Apple.

Wadau wamekua na shauku ya kutaka kujua ni kitu gani cha tofauti ambacho TECNO wameweza kukiongeza kwenye toleo hilo jipya.

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya http//www.tecno-mobile.com/tz

 

Comments are closed.