The House of Favourite Newspapers

Aston Villa Yanasa Mashine Mpya

0

ASTON VILLA imethibitisha kukamilisha usajili wa Bertrand Traore kutoka Lyon. Traore hapo awali alikuwa akiichezea Ajax na Chelsea kabla ya kusaini Lyon misimu mitatu iliyopita.

“Tunafurahi kwamba Bertrand amechagua kuja Villa, ni mchezaji aliye na kipaji kikubwa ambaye atazidisha ubora kwenye safu ya ushambuliaji,” amesema kocha mkuu wa Aston Villa, Dean Smit.

Traore amesaini Villa kwa ada inayoripotiwa kuwa Euro mil. 18.4 ambayo inaweza kuongezeka kwa kiwango cha uro mil. 2.2. Winga huyo mwenye umri wa miaka 25 alicheza mechi 126 kwenye mashindano yote na alifunga mabao 33 katika misimu mitatu na OL.

Leave A Reply