The House of Favourite Newspapers

ATCL Yasitisha Safari Zake Afrika Kusini

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL) limesitisha rasmi safari zake kati ya Dar es Salaam na Johanessburg, Afrika Kusini,  kuanzia Oktoba 7, 2019, na abiria ambao tayari walikuwa wamekata tiketi kwa ajili ya usafiri huo watarudishiwa nauli zao.

 

Taarifa iliyotolewa na ATCL Oktoba 3, 2019, na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Ladislaus Matindi,  iliwaelekeza mawakala wa tiketi wote kurejesha nauli za wateja hao ambao tayari walikuwa wamekata tiketi.

 

ATCL ambayo ilikuwa ikifanya safari hiyo mara nne kwa wiki (Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili) iliacha kufanya safari kati ya miji hiyo Agosti 23,2019 baada ya ndege yake aina ya Airbus A220-300 kuzuiliwa katika uwanja wa Oliver Tambo jiji Johannesburg kwa amri ya Mahakama Kuu ya Guateng.

 

Baada ya takribani wiki mbili ndege hiyo iliachiwa huru kwa uamuzi wa mahakama.

Comments are closed.