The House of Favourite Newspapers

Athanas Myonga Ashinda Tsh. Milioni 7 za Shindano la Stories Of Change 2023

0

Athanas Myonga amefanikiwa kuwa Mshindi wa kwanza katika Shindano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Jamii Forums ambapo Wananchi mbalimbali walipata nafasi ya kuandika maandiko yenye lengo la kusaidia jamiii katika Utawala Bora na Uwajibikaji.

Mshindi huyo amepata ushindi wa andilo lililolenga kutoa ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu kupanga Malengo ya Fedha zinazokusanywa, ambapo amejizolea kitita cha fedha taslimu Tsh. 7,000,000/-

Andiko lake linalopatikana ndani ya JamiiForums.com kwenye Jukwaa la Stories of Change, linasema “Namna ya kupanga malengo ya fedha za kukusanya TRA ili kuwe na uwajibikaji, sio kila Mwaka wanatuambia wamevuka lengo, kwa kujiwekea malengo madogo”

Mshindi wa kwanza katika Shindano la Stories Of Change 2023, Athanas Myonga akiongea baada ya kutangazwa.

Wengine waliokabidhiwa zawadi katika Usiku wa Tuzo uliofanyika Hyatt Regency Jijini Dar es a Salaam ni mshindi wa pili ni Respick Tairo Hugolini (Tsh. 4,000,000), Nathaniel Atanas wa tatu (Tsh. 3,000,000), wa nne ni Bashari Kidaya (2,000,000) na wa tano ni Nick Rusule (Tsh. 1,000,000).

Mgeni Rasmi alikuwa Balozi wa Sweden, Charlotta Ozaki, ambapo pia Mabalozi wengine walihudhuria ni Balozi wa Marekani, Dkt. Michael Battle Sr, Balozi wa Denmark – Mette Norgaard.

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Mobhare Matinyi amesema “Serikali ya Awamu ya 6 inatambua umuhimu wa kushirikisha Wananchi katika kuimarisha Utawala Bora Nchini hivyo tunatambua mchango wa JamiiForums kupitia Shindano la Stories of Change.

“Ni sehemu ya mkakati wa Serikali na imebainishwa katika Mkakati wa kuboresha Uchumi wa Kidijitali 2023-2033 na hata kwenye Rasimu ya Sera ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari ya 2023.”

Maxence Melo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji JamiiForums.

MKURUGENZI WA JAMII FORUMS
Maxence Melo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji JamiiForums amesema “Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wetu wa miaka 5 (2020-2024), tumedhamiria kuinua sauti za Wananchi na kuimarisha Upatikanaji wa Taarifa kama moja ya maeneo yetu muhimu ya kimkakati.

“Tunafanya hivyo kwa Mashirikiano na wadau wenye nia sawia ili kuongeza ubora wa maudhui mtandaoni hasa katika jukwaa la JamiiForums.”

Naye, Meneja Programu wa JamiiForums, Ziada Omary amesema “Huu ni Msimu wa Tatu wa Stories of Change tumepata maandiko 1,778 ambapo yaliyokidhi kuchapishwa ni 1,214 lakini tuzo zimetolewa kwa washindi bora watano, tunatambua mchango wa kila aliyeshiriki na kupendekeza Mabadiliko chanya na kuongeza idadi ya Maudhui ya Kiswahili yenye tija Mtandaoni.”

Leave A Reply