The House of Favourite Newspapers

Simba Yatamba Kuendeleza Rekodi Yake leo dhidi ya Singida Fountain Gate

0
Roberto Oliveira

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira, amesema kuwa wanahitaji kuendelea na rekodi zao za kupata matokeo mazuri kwenye mechi za ligi ikiwa ni pamoja na mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Singida Fountain Gate.

Leo Simba inatarajiwa kushuka uwanjani kwenye msako wa pointi tatu dhidi ya Singida Fountain Gate, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti, Singida.

Huu utakuwa ni mchezo wa 16 kwa Oliveira kwenye ligi kukiongoza kikosi cha Simba ambapo mechi 15 zilizopita, 13 alishinda na mbili aliambulia sare.

Kocha huyo amesema: “Tunahitaji kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu dhidi ya Singida Fountain Gate. Rekodi yetu ya kucheza bila kupoteza hiyo ni muhimu kuendelea na tunajua kuwa utakuwa mchezo mgumu.

“Kikubwa ni kutambua kwamba wachezaji wapo tayari na maandalizi ambayo tumefanya yanatupa nguvu ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu.”

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA, SPOTI XTRA

IGP WAMBURA APANGUA MAKAMANDA 3 wa POLISI – MKEKA WOTE HUU HAPA…

Leave A Reply