The House of Favourite Newspapers

Atupwa Jela kwa Kulawiti Mtoto

0

Octavian Kaijage (26) mkazi wa Kambarage Manispaa ya Shinyanga, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wa darasa la nne (11) (jina limehifadhiwa), ambaye anasoma Shule ya Msingi Kambarage Mjini Shinyanga.

Wakili wa Serikali Wampumbulya Shani, ambaye alikuwa akiisimamia kesi hiyo, amesema kijana huyo alitenda kosa hilo Novemba 23 mwaka juzi, ambapo hukumu yake imetoka jana kwa kufungwa miaka 30 jela, kesi iliyokuwa ikisikilizwa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya, Ushindi Swalo.

Amesema kijana huyo alikuwa na tabia ya kulawiti wanafunzi wa kiume, ambao wanasoma katika shule hiyo ya Msingi Kambarage, kwa kuwarubuni kwenda kucheza Game nyumbani kwake, na kisha kuanza kuwafanyia mchezo huo mchafu.

“Huyu kijana tabia ya kulawiti wanafunzi ndiyo ulikuwa mchezo wake, ambapo alikuwa akiwarubuni kwenda kucheza game nyumbani kwake, baada ya hapo anakwenda mwanafunzi Mmoja Mmoja na kuanza kumlawiti,” amesema Shani.

“Mwanafunzi huyu aligunduliwa na mjomba wake, sababu ya kutoroka nyumbani mara kwa mara, ndipo akambana kuwa hua ana kwenda wapi, na kusema kwa Octavian, na kwa vile kijana huyu ana julikana kwa michezo yake michafu, akamuuliza hua anakufanyaje na kumweleza ana muingiliaga kwa nyuma,” ameongeza Shani.

Leave A Reply