The House of Favourite Newspapers

Aucho Achota Mil 115 Yanga, Mchongo Mzima Upo Hapa

0

IMEFAHAMIKA kuwa, Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa zamani wa El Makkasa ya nchini Misri, Mganda, Khalid Aucho kwa dau la dola 50,000 (zaidi ya Sh 115.6Mil).

 

Yanga wamefanikiwa kumsajili kiungo huyo kwa mkataba wa miaka miwili ambapo Spoti Xtra lilikuwa likifahamu mchongo mzima hadi kukamilika kwake ambapo katika toleo la juzi Jumapili, stori kubwa ilitoka na kichwa cha habari kilichosomeka; Aucho mali ya Yanga.

Usajili wa Aucho unafikisha idadi ya wachezaji wapya sita ndani ya Yanga kuelekea msimu ujao ambao tayari wametambulishwa. Wengine ni Djigui Diarra, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Djuma Shaban na Yusuph Athumani.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Uganda na kuthibitishwa na mmoja wa mabosi wa Yanga, kiungo huyo amesaini mkataba huo kwa dau hilo nono.Kiungo huyo mwenye miaka 28, ni moja kati ya viungo bora wa chini katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

 

Aucho ni mzoefu wa michuano mikubwa akicheza ligi mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu ya Serbia alipokuwa akiitumikia Red Star Bergrade.Pia amewahi kukipiga Ligi Kuu ya India katika timu za East Bengal na Churchill Brothers.

 

Kiungo huyo amekipiga Ligi Kuu ya Afrika Kusini akiichezea Baroka FC, Misri (El Makkasa), Kenya (Tusker na Gor Mahia) na Uganda akicheza Simba FC.

 

Akizungumzia usajili wake, Aucho alisema: “Nimekuja Yanga kwa mapenzi yangu, sijafuata fedha.”Wakati huohuo, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa, amethibitisha wazi kwamba, wameachana na makipa wao, Metacha Mnata na Farouk Shikhalo.

Leave A Reply