The House of Favourite Newspapers

Mdogo wa Wema Adaiwa Kunaswa na Madawa, Aunt Amwaga Machozi (Picha + Video)

0

WAFANYABIASHARA wanne wa Dar es Salaam, wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin kilo 30.

 

 

Washtakiwa hao ni Joseph Dalidali(27), Said Mbasha (24) Mkazi wa Kinondoni, Allu Murugwa (24) (ambaye ni mdogo wa Msanii wa Bongo Movies, Wema Sepetu) mkazi wa Kijitonyama na Fatima Shomari (24).

 

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao, leo, Machi 11, 2021 na wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakim Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya.

 

 

Wakili Simon amedai kuwa washtakiwa wanakabikiwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 21/2021.
Kabla ya kusomewa mashtaka yao, Hakimu Isaya alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini( DPP).

Katika kusikiliza kesi hiyo alikuwepo muigizaji maarufu wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ambaye alimwaga machozi ndani ya chumba cha mahakama baada tu ya kufika na kuwaona watuhumiwa ambao inadaiwa ni watu wake wa karibu.

 

 

Akiwasome mashtaka yao, wakili Simon amedai kuwa Machi 3, 2021 katika eneo la Kijitonyama Wilaya Kinondoni, washtakiwa kwa pamoja walijihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 30.6, wakati wakijua ni kosa kisheria.

 

 

Shtaka la pili, linalomkabili Dalidali na Shomari, wanadaiwa Machi 3, 2021 katika eneo la Kinondoni mtaa wa Kasaba , washtakiwa hao wanadiwa kukutwa na gramu 2.63 za bangi, wakati wakijua kufanya biashara hiyo ni kosa kisheria.

 

 

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, upande wa mashtaka umedai upelelezi haujakamilika na ukaaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Isaya ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 24, mwaka huu.

 

Leave A Reply