The House of Favourite Newspapers

AUNT EZEKIEL: WEMA ALINIFANYA NIMJUE IYOBO

Tokeo la picha la aunt ezekiel

MAMBO yanazidi kunoga katika safu hii ya Siku ya Kwanza Kukutana, leo tunaye mrembo kutoka Bongo Movies, Aunt Ezekiel ambaye anasimulia jinsi alivyokutana na mzazi mwenziye, Mozes Iyobo: Kiukweli nampenda sana rafiki yangu kipenzi Wema Sepetu kwa sababu yeye ndiyo kiunganishi kati yangu mimi na kipenzi changu, Iyobo.

Miaka kadhaa iliyopita nilikwenda nyumbani kwa Wema nikamkuta kijana mmoja hivi, yes ndio Iyobo. Kiukweli sikujua kama itatokea siku moja tukawa wapenzi. Basi, tukawa tumepeana namba za simu tukawa tunawasiliana mwisho wa siku tukawa karibu. Kwa kile kipindi mimi sikuwa na mahusiano yoyote na Iyobo akawa anajaribu kutupa ndoana kwangu nikawa namzungusha zungusha, si unajua sisi wanawake hata kama umependa utajifanya kama vile hujapenda?Picha inayohusiana

Hivyo yani, akawa anaendelea kukumbushia suala lake basi nikaamua kuingia kwenye mahusiano mara penzi likanoga kupita kiasi. Kwa kweli siku zikaenda, nikabahatika kushika ujauzito. Watu wengi wakawa wananipigia simu kuulizia kuhusu mhusika wa ujauzito wangu. Mimi nikawa naendelea tu na maisha yangu basi ile siku ya ‘baby shower’ yangu, Iyobo alipokuja nikamtambulisha kuwa yeye ndio baba wa ile mimba watu hawakuamini. Kwa kweli sijajua kwa nini walikuwa hawaamini ikiwa yule ni mwanaume aliye kamili.

Kuna watu walitoka na kwenda kumwambia kuwa ule ujauzito siyo wake lakini namshukuru Mungu akampa uvumilivu mpaka miezi tisa nikajifungua mtoto wa kike, nikamuita Cookie. Kiukweli Mungu aliwaumbua wale waliokuwa wanaingilia maisha ya watu yule mtoto alifanana na baba yake kiasi ambacho mimi mwenyewe nilipata faraja sana kwa sababu yalizungumzwa mengi maana sisi mastaa kila mtu anatujua kivyake na kutuzungumza atakavyo yeye.Tokeo la picha la aunt ezekiel na wema

Ila niseme tu kiukweli nampenda sana mume wangu namuona kama bosi wangu, kingine ananisapoti kwenye kazi zangu za usanii na vile alivyo na mapenzi makubwa kwa mtoto wetu niseme tu yeye ni baba bora kwa Cookie. Maisha tunayoishi ni zaidi ya watu walio kwenye ndoa ila si kwamba sitafunga ndoa rasmi, Mwenyezi Mungu akitujalia tutafanya hivyo. Kikubwa Iyobo atambue kuwa nampenda sana yeye pamoja na binti yetu.

MUHIMU: Kwa mwenye simulizi yake tamu na namna alivyokutana na mpenzi wake, bila kujali ustaa, anaweza kutuma picha ya harusi yake na maelezo kwenye namba 0718 008 152.

Msimuliaji: Aunt Ezekiel Mwandishi: Neema Adrian

Comments are closed.