The House of Favourite Newspapers

AUNT LULU: DIAMOND OA SASA

Image result for aunt lulu
‘Aunt Lulu’

MTANGAZAJI Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ ameibuka baada ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kumsihi aoe sasa kwani ameshakua na kuoa kutamletea heshima zaidi.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Aunt Lulu alidai ameamua kumshauri staa huyo ambaye amekuwa akimpenda siku zote kutokana na kujituma kwake kikazi kwani si kila mwanamke ana nyota nzuri ya kumfanya aende mbali.

“Unajua ujana huwa hausubiri, kadiri unavyosherehekea siku yako ya kuzaliwa ndivyo uzee unavyokaribi, sasa kwa Diamond ili azeeke vizuri, angeoa sasa kwani Waswahili wanakwambia kubadilibadili wanawake nako huleta mikosi na kujikuta ukianguka moja kwa moja,” alisema Aunt Lulu.

 

Alimsisitizia kuwa endapo ataoa hata hao wanaopenda kujipendekeza kwake, watapungua kwani ndoa huheshimiwa.

STORI: Hamida Hassan, Dar

DIAMOND Ampa Bajaj Mama Mlemavu Tandale, Atoa Machozi

Comments are closed.