The House of Favourite Newspapers

Aunt, Wema wakiri kuvunja ndoa ya Petit

0

WAIGIZAJI Aunt Ezekiel na Wema Sepetu, wamekiri kuvunja ndoa ya meneja wa wasanii Petit Man na kumrejesha jamaa huyo kwenye himaya ya mke wa zamani, Esma Khan.

Warembo hao wamekiri kuivunja ndoa mpya ya Petit na Maimuna Adam ‘Queen Mai’ ambao wameachana hivi karibuni.

Akizungumza kwa niaba ya mwenzake, Aunt alisema, wao ndio waliosababisha ndoa ya awali ya Petit na Esma, kwa hiyo haoni tatizo kumrejesha kwa mara nyingine.

“Kwa wanaojua kwa undani, sisi tulimshawishi Petit amuoe Esma. Sasa kwa hiyo sio ajabu kumrejesha kwenye himaya yake ya awali na kuivunja ndoa yake mpya,” alisema Aunt.

Kwa upande wake Petit, ameweka wazi kwenye ukurasa wake wa Instagram picha ya Wema na Aunt na kisha kuwashukuru kuwa ndio waliomfanya avunje ndoa yake na Queen Mai kisha kurejesha majeshi kwa Esma.

“Aunt natoa shukrani kwako na mwenzako Wema nilipokuja kuwaomba ushauri mlisema nirudi kwa Esma, kwa kuwa kule sio saizi yangu, Mungu awaongoze,” aliandika.

Esma na Petit walioana kisha kufanikiwa kupata mtoto mmoja na kuachana kwa talaka kabla ya kurejesha upya penzi lao hivi karibuni.

STORI: IMELDA MTEMA, RISASI

Leave A Reply