The House of Favourite Newspapers

Aunty Lulu agida bia asubuhi

0

IMG_3291Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ akipiga mtungi huku akijilipua na fegi.

Na Gladness Mallya, RISASI mchanganyiko
DAR ES SALAAM: Mwanadada asiyeishiwa matukio mjini, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ hivi karibuni alinaswa akigida bia na kuvuta sigara asubuhi na mapema, akionekana kukaidi agizo la Rais John Joseph Magufuli la kuwataka watu kuachana na tabia ya kunywa pombe saa za kazi.

Paparazi wetu alimnasa Aunty Lulu ndani ya baa ya Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo alikuwa anakunywa bila wasiwasi huku akishushia na kuvuta sigara hali iliyosababisha watu kumkodolea macho huku wengine wakijadili amekuwaje siku hizi kulewa asubuhi tena muda wa kazi.

“Jamani Aunty Lulu amebadilishwa na nini maana siyo mara ya kwanza kumuona anakunywa muda wa kazi huku akivuta sigara kwa wingi, hilo pakti la sigara analotembea nalo atamaliza kuvuta sasa hivi,” alisema mtu mmoja aliyekuwa akinywa supu katika baa hiyo, wakati msanii huyo akipuliza moshi bila woga.

IMG_3288Baada ya paparazi wetu kumpiga picha za kutosha, alimfuata Aunty Lulu na kumuuliza kulikoni kunywa pombe muda wa kazi na kukiuka maagizo ya rais ambapo alisema;
“Unajua siku hizi nafanya kazi ya biashara ya kusafiri mikoani hivyo siku ambayo napumzika kama hivi nakunywa kuanzia asubuhi ili kutuliza mawazo, hizi sigara navuta ili kupunguza mwili maana niliambiwa na watu kwamba zinapunguza unene, nataka kurudi kuwa miss kama zamani.

“Agizo la rais sijalisikia bado lakini najua hapa sijavunja sheria maana si unajua kila mtu ana siku yake ya mapumziko na mimi leo niko mapumziko ndiyo maana nakunywa saa hizi.”

Leave A Reply