The House of Favourite Newspapers

Mwenyekiti wa Chadema Iringa Vijijini, Apata Ajali na Kufariki

0

1Ajali hiyo ilivyotokea.1qSinkala Mwenda wakati wa uhai wake

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Iringa Vijijini,  Bw. Sinkala Mwenda amepata ajali jana  jioni  eneo la Tanangozi na kukimbizwa Hospitalini kwa ajili ya kunusuru maisha yake jambo ambalo lilishindikana baada ya kufariki dunia muda mfupi wakati madaktari wakijitahidi kuokoa uhai wake.

Sinkala Mwenda alikua Mwanasheria Kijana Msomi wa CHADEMA. Mwenda alikuwa mgombea kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga 2014 ambaye aliwashinda wagombea wengine 12 katika kura za maoni ndani ya chama, alipokwa ushindi na chama hicho na kikamteua mshindi wa pili Grace Tendega kupeperusha bendera katika uchaguzi mdogo huo. Kwa sasa alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Iringa Vijijini

Pumzika kwa amani Sinkala Mwenda!

Leave A Reply