The House of Favourite Newspapers

Aunty Lulu Atoboa Siri Ya Kujiachia Viwanja

Mtangazaji Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.

ALIYEKUWA mtangazaji Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kila kukicha amekuwa akionekana akijiachia viwanja mbalimbali akila bata ambapo ameibuka na kutoboa siri za jeuri inayomfanya anajiachia hivyo.

 

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Aunty Lulu alisema siri ya kujiachia viwanja ni kutokana na maisha yake kumnyookea tangu alipookoka kwani amepata mafanikio kwa sababu kila anachokifanya kinakwenda vizuri hasa biashara zake ambazo zinamuingizia kipato tofauti na zamani alikuwa akitegemea wanaume.

 

“Kiukweli nimeona faida za kumuomba Mungu kwani kwa sasa mambo yangu yanaenda vizuri siyo ya wanaume tena kama zamani, nimekuwa nikifanya biashara zangu zinanilipa na ndiyo maana muda mwingine natoka na kwenda kupunga upepo ufukweni au kwenye hoteli nzuri kwa ajili ya kupumzisha akili na sina mambo ya wanaume tena,” alisema Aunty Lulu.

Comments are closed.