The House of Favourite Newspapers

Aussems: Yanga haiwezi kuzuia Ubingwa wa Simba

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amewachimba mkwara wapinzani wake, Yanga katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kusema kuwa, hata wafanye jambo gani, hawawezi kuwazuia kutetea ubingwa wao msimu huu, kwa kuwa wamejipanga kutimiza jambo hilo.

 

Yanga ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 64, ikifuatiwa na Azam wenye pointi 53 huku Simba ikiwa na pointi 48 kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Stand United uliopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Aussems alisema kuwa kwa sasa wanachokiangalia ni kushinda mechi zao zilizabakia ili kuweza kufanikisha malengo yao ya kutetea ubingwa.

 

“Tunachokiangalia sisi ni kuweza kutwaa ubingwa msimu huu bila ya kujali nani yupo mbele yetu, niliwahi kusema hatuwezi kuwa mabingwa kama hatujawafunga Yanga na Azam ambao tayari wote tumeshawafunga.

 

“Ratiba yetu imekuwa ngumu kutokana na mechi kuwa karibu sana lakini hatuna sababu ya kukataa tamaa kwa sababu dhamira yetu sisi ni kutetea ubingwa na hatuoni mtu anayeweza kuzuia jambo hilo kwa kuwa malengo yetu ni kuendelea kushiriki michuano ya kimataifa kama ilivyo sasa,” alisema Aussems.

IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Comments are closed.