The House of Favourite Newspapers

HATIMAYE RUGE AZIKWA KISHUJAA BUKOBA – PICHAZ

Mtoto wa marehemu Ruge akiwa mashada katika kaburi la marehemu baba yake ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba.

HATIMAYE mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba umezikwa Machi 4, 2019 kishujaa nyumbani kwao katika kijiji cha Kiziru Kata ya Karabagaine Wilaya ya Bukoba na hakuna mahubiri yaliyotolewa na katibu huyo.

Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga, aakiweka mashada katika kaburi la marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa jana kijijini kwao Kiziru Bukoba.

Zoezi la kuzika mwili wa Ruge lilianza kwa Ibada ya mazishi ambayo iliongonzwa na Katibu wa Parokia ya Itahwa, Anatory Kyatwa huku nyimbo za kihaya zikipamba tukio la mazishi.

Wazazi, familia,  wakiweka mashada katika kaburi la marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa kijijini kwao Kiziru Bukoba.

Hii ilikuwa ni baada ya salamu za mwisho na kuagwa katika Viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba kabla ya kuzikwa kijijini kwao.

RC Makonda akiweka shada katika Kaburi la Ruge.

Baada ya kuongoza taratibu za kuweka mwili kwenye kaburi huku nyimbo zenye ujumbe wa neno la Mungu zikiendelea, umefuata utaratibu wa kuweka mashada ya maua.

Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, January Makamba akiweka shada.

Miongoni mwa walioweka mashada ya maua ni Wabunge akiwemo, Nape Nnauye na Wilfred Lwakatare pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Awali wakati wa tukio la kuaga mwili wake katika viwanja vya Gymkhana, Maaskofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba walimtaja Ruge kama kijana jasiri mzalendo na mfano wa kuigwa.

Askofu Desderius Rwoma ameitaka jamii kuenzi mambo mema aliyoacha huku msaidizi wake, Methodius Kilaini akisema vijana wengi wamepata mafanikio kutokana na udhubutu wake na ujasiri wa kusimamia anayoamini.

 

Mama wa marehemu Ruge Mutahaba (wa pili kushoto), akifuatiwa na mumewe wakiwa na aliyekuwa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala, dakika chache kabla ya mwili wa mtoto wao marehemu Ruge Mutahaba Kuingizwa kaburini, kijijini Kiziru. Rip Ruge

 

 

 

 

Comments are closed.