The House of Favourite Newspapers

Australia: Bawa lililookotwa Pemba ni la Ndege ya Malaysia

0

bawa la ndege (2) SERIKALI ya Australia jana Ijumaa, Julai 29, ilitoa tamko kupitia Wizara ya Miundombinu na Usafirishaji ya nchi hiyo kuwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa kipande cha bawa la ndege kilichookotwa katika kisiwa kidogo cha Kojani, Pemba, Zanzibar Mei 2016, ni cha ndege ya Malaysia Airlines, namba MH370 iliyopotea.

bawa la ndege (3)Ndege ya Malaysia Airlines, MH370 ilipotea Machi 2014 ikiwa na abiria na wafanyakazi wa ndege hiyo jumla yao ikiwa ni 239 wakati ikitokea Kuala Lumpur, Malaysia kuelekea Beijing, China.

Tafiti zilizofanywa na wataalam wa masuala ya ndege na anga huko Australia zimebaini kuwa huenda kuna mtu aliyezima kifaa cha mawasiliano (redio) cha ndege hiyo kabla ya kuanguka na kupotea kwenye Bahari ya Hindi.

bawa la ndege (1)Akizungumzia hilo,  Waziri ya Miundombinu na Usafirishaji wa Australia, Darren Chester, alisema bawa la ndege lililookotwa Pemba limefanyiwa utafiti Australia.

“Kuna uwezekano mkubwa kuwa kipande cha bawa la ndege kilichopatikana hivi karibuni nchini Tanzania ni cha ndege ya  Malaysia Airlines, MH370,” alisema waziri huyo.

“Matarajio yetu ni kuendelea kutafiti, kuona kama tutabaini taarifa zingine kutoka kwenye kipande hicho cha bawa la ndege,” alimalizia kusema Darren.

Watafiti wamebaini pia kuwa kipande cha bawa la ndege kilichookotwa visiwa vya Ufaransa mnamo Julai 2015 ni cha ndege ya hiyo hiyo ya  Malaysia Airlines, MH370.

Wameongeza pia kuwa, kuna vipande vingine kadha ambavyo vimeokotwa Msumbiji,  Afrika Kusini na Kisiwa cha Rodrigues kilichopo Mashariki mwa Mauritius, vipande vyote hivyo vinasadikika kuwa ni vya ndege hiyo iliyopotea.

Utafutaji wa mabaki ya ndege nyingine ya Boeing 777 unaendea katika Bahari ya Hindi kwa zaidi ya miaka miwili sasa, japo hakuna chochote kilichopatikana mpaka sasa.

Source: Reuters

Leave A Reply