The House of Favourite Newspapers

Aveva Afika Mahakamani Huku Hali Yake Ikiwa Tete – Video

Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva ambaye alikuwa akiugua kwa muda mrefu, leo Aprili 5, amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhudhuria kesi yake inayomkabili licha ya hali yake kuonekana imedhoofika huku akishikwa mkono kumsaidia kutembea.

 

Akiwa mahakamani hapo, muda mwingi alionekana kusaidiwa na makamu wake Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu ambaye ni mtuhumiwa mwenzake katika kesi hiyo ambapo wawili hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, nyaraka na kutakatisha fedha kiasi cha Dola za Marekani 300,000.

 

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka umeiomba mahakama kusogezwa mbele kesi ili kubadili hati ya mashtaka na kuongezwa mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo. Aidha, mahakama imeahirisha kesi hadi April 12, mwaka huu.

Aveva Afikishwa Mahakamani Akiwa na Hali Mbaya

Comments are closed.