The House of Favourite Newspapers

Aweso amtumbua Mkurugenzi Mamlaka ya Maji Kasulu

0

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) amemuondoa kwenye nafasi yake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kasulu, Eng. Riziki Andrew Nyamtega.

Aweso amechukua hatua hiyo kupitia mamlaka aliyonayo kupitia Sheria Na. 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019.

Aweso amewataka Wahandisi wa maji nchini kuhakikisha wanasimamia vema majukumu yao na kueleza kuwa hatovumilia yeyote ambaye ataonekana kutotekeleza majukumu yake kwa ufasaha katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma ya majisafi, salama na ya kutosheleza.

Leave A Reply