The House of Favourite Newspapers

AY, Nyashinski Kwenye Ngoma Moja

0

msanii-ay Rapa AY.

Gabriel Ng’osha, Gazet La Amani, Toleo La Alhamisi Jan. 19, 2017

MSANII wa Bongo Fleva, Ambwene Yessayah ‘AY’ wiki hii anatarajia kuachia wimbo mpya akiwa amemshirikisha msanii nguli kutoka Kenya, Nyamari Ongegu ‘Nyashinski’ ambaye aliwahi kutamba na wimbo wa Tuendelee au Tusiendee na Swing Swing akiwa na Kundi la Kleptomaniax.

nyashinskiMsanii Nyashinski.

Akizungumza na Gazeti la Amani, AY amesema kuwa ameamua kumshirikisha nguli huyo kwa sababu anamuamini katika uwezo wake wa kuimba na kurap kama alivyo yeye.

“Nyashinski ni msanii nguli kwa Kenya, kitambo sana nilitamani kufanya naye ngoma lakini ikashindikana, kwa bahati nzuri dili hilo limefanikiwa hivi karibuni na wiki hii ninaachia wimbo nikiwa naye na nitafanya mpango wa kumleta Bongo kumtambulisha, ni mapema mno kutaja jina la wimbo huo lakini mashabiki wangu watarajie kitu kizuri na naamini wataupenda,” alisema AY.

Leave A Reply