Azam FC Kutumia Mbinu za Mazembe Kuiua Simba SC

UWEZO ulioonyeshwa na kikosi cha Azam FC kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe, umelifanya benchi la ufundi la timu hiyo kuamini sasa wako tayari kwa mchezo wa kiporo cha Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

 

Azam FC, juzi Jumanne ilionyesha kiwango bora licha ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar, kesho Jumapili.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Zakaria Thabith ‘Zaka za Kazi’ alisema kikosi hicho kimeanza rasmi kambi ya kujiandaa na mchezo huo jana Alhamisi baada ya likizo ya siku moja.

“Kocha Mkuu George Lwandamina ameridhishwa na kiwango ambacho kikosi kimeonyesha katika michezo yote mitano ya kujipima nguvu kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Bara.

 

“Mchezo uliopita dhidi ya Mazembe umempa taswira kamili ya utayari wa wachezaji wake kuelekea mchezo ujao wa ligi dhidi ya Simba.“

Tayari tumeanza rasmi maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Simba leo (jana) Alhamisi, baada ya likizo ya siku moja, ambapo tumejipanga kutumia mchezo huo kurejea tena kwenye ushindani, tunajua msimu uliopita hatukupata matokeo dhidi yao hivyo hatutaki kuona hilo likijirudia,” alisema Zaka.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

UWOYA Avunja UKIMYA Ishu ya H BABA – “NATAMANI KUWA MCHUNGAJI SIKU MOJA”

Toa comment