The House of Favourite Newspapers

Azam FC Yamng’oa Kocha Moalin Pamoja na Msaidizi Wake, Wapewa Majukumu Mapya

0
Azam imefikia makubaliano ya kuchana na aliyekuwa Kocha Mkuu Abdihamid Moalin

KLABU ya Azam FC imefikia makubaliano ya kusitisha kandarasi ya Kocha wake Mkuu Abdihamid Moalin pamoja na na msaidizi wake Omary Nasser.

 

Kupitia katika ukurasa rasmi wa mitandao ya kijamii ya klabu hiyo imebainisha kuwa Makocha hao wameachia ngazi katika nafasi za ukocha wa timu ingawa bado wataendelea kuwepo ndani ya klabu hiyo kwa kupangiwa majukumu mengine.

Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Azam FC Omary Nasser

“Tumefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wetu, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser, kuachia ngazi kama kocha mkuu na msaidizi mtawalia.

Hata hivyo, makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi klabuni kwetu katika nafasi nyingine ambazo tutazitangaza hapo baadaye.

Kwa sasa timu itakuwa chini ya Daniel Cadena, ambaye ni kocha wa makipa, hadi tutakapotangaza kocha mpya.

Cadena ni kocha mwenye leseni ya juu kabisa ya ukocha, UEFA Pro License.” Imesema taarifa kutoka klabu ya Azam.

Leave A Reply