The House of Favourite Newspapers

Watu 32 Wauawa na Wengine 159 Wajeruhiwa Tripoli, Libya

0
Mpambano kati ya makundi hasimu na yanayounga mkono Serikali nchini Libya yamesababisha mauaji ya watu wengi katika mji wa Tripoli

WATU 32 wameuawa na wengine 159 kujeruhiwa katika mapiganao kati ya makundi hasimu dhidi ya makundi yanayounga Serikali ya Libya ambapo yaliyotokea katika Mji wa Tripoli nchini humo.

 

Wizara ya afya ya nchi hiyo imesema kuwa familia 64 zimelazimika kuhamishwa kutoka kwenye maeneo yanayozunguka mapigano hayo.

 

Wizara hiyo imebainisha kuwa vituo vya matibabu vilivyopo katika mji mkuu vilipigwa makombora na magari ya kubeba wagonjwa yalizuiliwa kubeba raia huku kitendo hicho kikitajwa kuwa ni uhalifu wa kivita.

Waziri Mkuu wa Libya, Abdulhamid Dbeibah

Taarifa zinaeleza kuwa huduma za dharura zinaendelea kuwaokoa watu waliojeruhiwa na waliokwamba katika mapigano hayo.

 

Mapigano kati ya kundi hasimu na kundi linalounga mkono Serikali ya Libya yalitokea usiku wa kuamkia Ijumaa na kuhusisha makundi yanayounga mkono Serikali ya Umoja wa Kitaifa mjini Tripoli.

 

Mapigano hayo yanaongozwa na Waziri Mkuu, Abdulhamid Dbeibah na wafuasi wa Fathi Bashagha, ambaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu na bunge lenye makao yake Mashariki mwa Libya.

Miili ya watu waliouawa katika shambulio hilo

Hadi kufikia jana Jumapili, hali ya utulivu ilikuwa imerejea mjini Tripoli, lakini ghasia hizo zimeongeza wasiwasi wa kutokea mgogoro mkubwa zaidi tangu kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mnamo mwaka 2020.

 

Dbeibah amewashutumu wapinzani wake kwa kuendesha vita dhidi ya mji mkuu kwa vifaru na silaha nzito, huku Bashagha naye akimtuhumu Dbeibah kutaka kung’ang’ania madaraka kwa gharama yoyote.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave A Reply