The House of Favourite Newspapers

AZAM FC YAPATA STRAIKA MPYA KUTOKA GHANA

0
Mshambuliaji Bernard Arthur (kushoto)  amesainiwa na Klabu ya Azam FC Akitokea Liberty Professional ya Ghana

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, umefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji Bernard Arthur, akitokea Liberty Professional ya Ghana.

Arthur amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na matajiri hao kutoka viunga vya Azam Complex, na zoezi zima limefanikishwa na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohammed, aliyekuwepo nchini Ghana kukamilisha usajili wake.

Usajili wa Arthur, 20, ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo kwenye usajili huu wa dirisha dogo, anayekuja kuziba pengo la straika mwingine, Yahaya Mohammed, aliyeondoka kwa makubaliano maalumu ya pande mbili wiki chache zilizopita.

Stori na Esther Msofe ,GPL

Leave A Reply