The House of Favourite Newspapers

ALICHOKISEMA MBOWE KUHUSU WANACHAMA WAKE KUHAMIA CCM (VIDEO)

0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amesema uamuzi uliochukuliwa na baadhi ya wanachama waliotangaza kukihama chama hicho na kwenda Chama cha Mapinduzi (CCM), ni wa kawaida katika siasa na kuwatakia kila la heri huko waendako.

 

Akizungumza na mwandishi wa Mtandao wa Global Publishers, Mbowe amesema baadhi ya watu huamini kwamba wakiingia Chadema, kwa sababu wametoka kwenye chama fulani wakiwa na nyadhifa fulani, basi wakiingia Chadema tu watapewa vyeo, madaraka au mishahara mizuri.

 

“Lazima ujue kwamba chama kinajengwa na watu na kuna watu waliokipigania Chadema mpaka kikafikia hapa kilipo, inategemea unakuja wewe watu wanakuamini kwa kiasi gani na wanakupa nafasi ipi uitekeleze,” alisema Mbowe huku akimtolea mfano Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bavicha kwamba alikuwa na cheo ndani ya chama na bado amehama kwa hiyo siyo wote wanahama kwa sababu ya kukosa vyeo.

 

Mbowe aliongeza kwamba watu wanaotegemea kwamba wakiingia Chadema watakutana na neema ya vyeo na mishahara, hawawezi kudumu ndani ya chama hicho kwa sababu wanachama wa kweli wa Chadema wanajitolea, wanafanya kazi katika mazingira magumu ambayo yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu na kujituma,” alisema Mbowe na kuongeza kuwa ndani ya Chadema hawatazami maslahi bali kujenga chama.

 

Aliongeza kuwa japokuwa wameumizwa kiasi na uamuzi huo, Chadema haiwezi kuyumba kwa sababu imeshazoea kupitia kwenye misukosuko mikubwa ambayo inatengenezwa kwa makusudi kwa ajili ya kuiyumbisha, akitolea mfano wa tukio la kupigwa risasi kwa Lissu kwamba lilikuwa ni miongoni mwa vikwazo ambavyo chama hicho kinavipitia lakini kamwe hawawezi kurudi nyuma.

Leave A Reply