The House of Favourite Newspapers

AZAM INAZIDI KUWANASA TU, ANAFUATA JUMA ABDUL LEO

WAKATI kiungo mshambuliaji wa Singida United Mzimbabwe, Tafazwa Kutinyu akitambulishwa Azam FC, timu hiyo imepanga kumtambulisha leo beki wa Yanga, Juma Abdul.

Abdul ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika Yanga mwishoni mwa msimu pamoja na wachezaji wengine tisa, akiwemo Obrey Chirwa na Hassan Kessy. Huyo ni mchezaji wa pili wa Yanga kwenda Azam baada ya hivi karibuni kukamilisha usajili wa mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, timu hiyo itamtambulisha Abdul baada ya mkataba wake kumal­izika rasmi Ijumaa iliyopita.

Mtoa taarifa wetu alisema, Azam imepanga kufanya usajili bora wa kisasa kwa wachezaji wenye uzoefu katika kukiimari­sha kikosi chao ili kiweze ku­chukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao.

“Timu yetu imepanga kutam­bulisha baadhi ya wachezaji kesho (leo) Jumatatu kwa wale ambao tumefikia nao muafaka wa kuwasajili.

 

“Kati ya wachezaji ambao tumepanga kuwatambulisha ni Abdul, ni baada ya mkataba wake kumalizika rasmi Ijumaa iliyopita,” alisema mtoa taarifa huyo. Meneja Mkuu wa timu hiyo, Philip Arlando, alipotafutwa kuzungumzia hilo, alisema kuwa: “Tumepanga kutambulisha wachezaji baadhi tuliowasajili kesho (leo) Jumatatu.

 

“Nisingependa kuwaweka wazi wachezaji hao tutakaowatam­bulisha hivi sasa, hivyo kikubwa tusubirie siku hiyo ifike itajulikana, niseme kuwa tutafanya usajili mkubwa.”

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Comments are closed.