The House of Favourite Newspapers

Azam kuifanyia umafia Triagle United

Image result for azam fc Ethiopia 3-2

AZAM FC ambayo imefanikiwa kutinga hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho imeanza kufanya umafia baada ya kuwa kwenye mchakato wa kupeleka shushushu Zimbabwe kwa ajili ya kwenda kuwafuatilia wapinzani wao.

Azam imefanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Fasil Kenema ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-2, walianza kwa kufungwa ugenini bao 1-0 kisha nyumbani wakashinda mabao 3-1.

 

Image result for azam fc Ethiopia 3-2

Sasa Azam inatarajia kukutana na Triagle United katika mchezo wa hatua ya kwanza ya michuano hiyo iliyopangwa kupigwa kati ya Septemba 13-15, huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 27-29, mwaka huu.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ ameliambia Championi Jumamosi kuwa, uongozi umeamua kutuma mtu kwa ajili ya kuwafuatilia wapinzani wao Triagle United katika mchezo wao wa ligi kuu ili kujua mbinu zao kabla ya kuwakabili.

“Mchezo huu tunauchukulia umuhimu wa hali ya juu, tunatarajia kutuma mtu kwa ajili ya kwenda kufuatilia mechi ya ligi ya wapinzani wetu ili kujua mbinu zao ikiwa ni pamoja na kuwafuatilia kupitia video zao.

“Mchezo huo tunauchukulia umakini wa hali ya juu ili tuweze kufanikiwa kusonga mbele, tunahitaji kushinda mchezo huo, hivyo tunachukua nafasi hii kuweza kujiandaa ipasavyo.

“Ungozi unajipanga vyema katika nafasi yake kuhakikisha unampa ushirikiano wa hali ya juu kocha, Etienne Ndayiragije ili kuweza kufanikiwa kufanya vyema katika mashindano haya,” alisema Popat.

 

Comments are closed.