The House of Favourite Newspapers

Azam Waweka Rekodi Dar

ACHANA na matokeo, lakini Azam FC wameweka rekodi na heshima ya aina yake kwa kuchezesha wachezaji saba kwenye mechi dhidi ya Simba ambao wamewatengeneza wenyewe pale Chamazi.

 

Wachezaji hao saba wamekulia kwenye kituo cha kukuza vipaji cha timu hiyo yenye uwanja wake wa kisasa wa Azam Complex.

Simba asilimia kubwa ya wachezaji wao wamenunua kwa gharama kubwa kutoka ndani na nje ya nchi. Walioanza kwenye kikosi cha kwanza ni kiungo Mudathir Yahya, winga Joseph Mahundi ambao wote walionyesha kiwango. Lakini mastaa wengine watano walikuwa benchi wamekulia Azam na wameiva kwa kucheza mechi zozote kubwa.

 

Hao ni kipa Benedict Haule, mabeki Abdul Omary, Oscar Masai, kiungo Masoud Abdallah na mshambuliaji Shaban Chilunda. Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Azam imepewa zawadi ya mamilioni ya shilingi na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kama kuwapongeza kwa program zao makini za kukuza vijana.

Comments are closed.