The House of Favourite Newspapers

Ligi Kuu ya Serengeti Lite kutimua vumbi leo

Afisa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Brewerieas (SBL) George Mango (katikati) akizungumza na waandishi wa habari.

 

Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite Msimu wa 2019/2020, inatarajia kuanza kutimua vumbi rasmi leo Jumamosi Oktoba 26, 2019 kwenye Viwanja 6 tofauti. Ligi hiyo inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Lite itashirikisha timu 12,zitakazocheza mtindo wa nyumbani na ugenini. Katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite timu mbili zitakua zinashiriki kwa mara kwanza baada ya kupanda Daraja.

Timu zilizopanda Daraja ni Ruvuma Queens ya Ruvuma na TSC Queens ya Mwanza. Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake, Amina Karuma amesema Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite inaendelea kuwa bora na kuimarika katika kila msimu.

Karuma amepongeza udhamini wa SBL kupitia Kinywaji cha Serengeti Premium Lite ambao  umekua chachu ya kuongeza mvuto Pamoja na kuvutia vipaji vipya katika soka la wanawake.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wanawake (TWFA) Amina Karuma (katikati) akizungumza na waandishi wa habari.

 

Naye Ofisa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa Ligi hiyo, George Mango amesema wanaamini msimu huu wa 2019/2020 utakua wa aina yake katika ushindani na hamasa.

“Serengeti Breweries Limited kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lite imewekeza kiasi cha Shilingi milioni mianne ma hamsini (Sh 450 milioni) ili kuwezesha ligi ya wanawake kuwa ya ushindani mkubwa na kuwaletea msisimko mashabiki wa soka,” alisema George na kubainisha kwamba maandalizi ya kuwezesha michuano hiyo yamekamilika.

Mango aliongeza; “pamoja na kutoa burudani safi kwa mashabiki, udhamini wetu katika michuano hii unalenga kuonyesha kuwa wanawake ambao mara nyingi wamekuwa wakiachwa nyuma kwenye michezo na haswa soka, wanaweza kufanya vizuri endapo wanawekewa mazingira wezeshi.”

Baadhi ya waandishi wa habari, wakifuatilia mkutano wa kutangaza kuanza kwa Ligi ya Wanawake.

Afisa huyo  alisema kuwa, tangu kuanza kwa udhamini huo, idadi ya wanawake wanaojiunga na kushiriki mchezo wa soko imekuwa ikiongezena nchini na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya hali ya juu vya soka kutoka kwa wanawake.

Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji cha Serengeti Lite imeweza kuwekeza jumla ya Sh450 Milioni kama udhamini wa ligi hiyo ya wanawake nchini kwa kipindi cha miaka mitatu.

Timu Za Ligi Kuu Ya Wanawake (SWPL)

 

  1. Kigoma Sisterz- Kigoma
  2. Simba Queens – Dsm
  3. Alliance Girls –Mwanza
  4. Baobab Queens – Dodoma
  5. Mlandizi Queens – Pwani
  6. Jkt Queens – Dsm
  7. Panama – Iringa
  8. Ruvumaqueens –Ruvuma
  9. Marsh Academy – Mwanza
  10. Tsc Queens – Mwanza
  11. Yanga Princess –Dsm
  12. Tanzanite – Arusha.

 

Imeandaliwa na Neema Adrian/GPL

 

Comments are closed.