The House of Favourite Newspapers

Azania group of companies yaja na mpya

0
Group Business Developer, Joel Laizer akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Kampuni ya Azania Group baada ya kutimiza malengo ya mwaka 2020 kufikia kusambaza bidhaa zake mikoa tisa hapa nchini wameendelea kuzalisha bidhaa zao kwa ubora wa hali ya juu huku zikiwa na gharama nafuu. Akizungumza na waandishi wetu Group Business Developer, Joel Laizer, Bidhaa hizo ni pamoja na sabuni za King Limau na Marhaba ambazo hazichubui mikono kama zilivyo sabuni zingine ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na watumiaji.

“Baada ya bidhaa hizo sasa tuna unga wa ngano ambao una ubora wa hali ya juu kuliko unga wa ngano unaopatikana sehemu nyingine yeyote”. Alisema Joel. Pamoja na unga huo Azania imetoa mafuta yenye ubora wa hali ya juu ambayo huchujwa mara tatu na mashine kutoka Bara la Ulaya na hivyo kuwa na kiwango cha Ulaya.

HABARI: NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL 

Leave A Reply