The House of Favourite Newspapers

Aziz Ki Atua Na Mabao Ya Guede Yanga

0
Joseph Guede (katikati)

MABOSI wa Yanga wana matumaini makubwa na mshambuliaji wao mpya, Joseph Guede huku ukiamini kuwa nyota huyo atafaidika zaidi mara atakaporejea kiungo Mburkinabe, Stephen Aziz Ki.

Kiungo huyo muda wowote kuanzia jana alitarajiwa kutua nchini kwa ajili ya kuuwahi mchezo wa ligi kuu dhidi ya Prisons Jumapili hii baada ya kuondolewa katika Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) akiwa anaichezea nchi yake ya Burkina Faso.

Aziz Ki ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa amefunga mabao 10 akifuatiwa na Jeane Balake aliyekuwa anaichezea mwenye 8 sawa na Feisal Salum anayeichezea Azam FC.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa licha ya mshambuliaji huyo kutofunga katika michezo miwili ya ligi, lakini ameonyesha vitu vichache ambavyo uwanjani vinavyowapa matumaini ambavyo kukokota mpira na umiliki wa mpira na kupiga pasi zinazofika kwa wachezaji wenzao.

Kamwe alisema kuwa anaamini ujio wa Aziz Ki, kutamfaidisha mshambuliaji huyo wakicheza pamoja katika safu ya ushambuliaji kutokana na ubora wake wa kupiga asisti ambapo msimu huu hadi sasa anazo mbili na mabao 10 akiwa ndiye kinara.

Aliongeza kuwa kurejea kikosini kwa Aziz Ki, kutatengeneza kombinesheni nzuri ya ushambuliaji pamoja na Guede hivyo mabeki wa timu pinzani wajiandae kupata ushindani watakapokutana katika michezo ijayo ya ligi.

“Ujio wa Guede kutaipa faida kubwa timu yetu ya Yanga, katika kutetea Ubingwa wetu wa ligi tuliouchukua ndani ya misimu miwili mfululizo iliyokuwa na mafanikio makubwa kwetu.

“Huyu Guede atafaidika sana, mara atakaporejea Aziz Ki kikosini, kwani ni mchezaji mwenye uwezo wa kupiga pasi za mabao, kikubwa wapinzani wajiandae,” alisema Kamwe ambaye aliongeza kuwa:

“Djigui Diarra na Azizi Ki wanatarajiwa kurejea ndani ya Yanga baada ya kumalizika kwa mechi dhidi ya Dodoma Jiji hivyo katika mchezo wetu unaofuata wa ligi tutakuwa nao hawa wachezaji wetu wawili muhimu.

“Kama unavyofahamu safari hii kuna timu zimetuzoea sasa tuwaambie tu kuwa tutaanza kutoa dozi zetu zile nzito kama ambavyo imekuwa kawaida yetu, muda si mrefu Wananchi wakae kwa kutulia kwani Yanga hii imedhamiria kufanya mambo makubwa mno.”

STORI: WILBERT MOLANDI na Marco Mzumbe

SAKATA la LISSU KUKATAZWA REDIONI – MAKONDA AMVAA VIBAYA – “ANALILIA REDIO – WATU wa KULIALIA TU”…

Leave A Reply