The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kufananisha na ‘Sikio la Kufa’, Barabara ya Mabatini Yawekewa Changarawe

1-eneo-la-miundombinu-hiyo-lililokuwa-korofi-katika-barabara-ya-kijitonyma-polisi-mabatini IKIWA ni takribani siku 10 baada ya Mtandao huu kuripoti kupitia Mjumbe wa Mtaa wa Polisi Mabatini, jijini Dar es Salaam, Steven Jovin kuwa barabara inayopita karibu na Kituo cha Polisi Kijitonyama (Mabatini) kufananisha na ‘sikio la kufa’, sasa barabara hiyo imewekewa changarawe eneo lililokuwa korofi.

Kamera yetu imefanikiwa kupita eneo hilo mapema hii leo na kunasa baadhi ya picha zinazoonesha sehemu hiyo ya miundombinu iliyokuwa korofi ikiwa imewekwa changarawe.

3Barabara hiyo ikiwa inarekebishwa

Baadhi ya wananchi waliupongeza mtandao huu kwa kufichua maovu mbalimbali pamoja na kero. Hamidu Iddi alisema amefurahishwa kutokana na kero hiyo kuondoshwa na sasa amewaomba wahusika wasiishie kuweka changarawe bali waweke lami.

1.Gari likipita eneo hilo kwa tabu.Barabara hiyo kabla ya kurekebishwa

Mnamo Septemba 1 mwaka huu, mtandao huu uliandika habari iliyokuwa na kichwa cha habari Miundombinu ya Barabara Polisi Mabatini, Dar… Sikio la Kufa! 

PICHA NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.