The House of Favourite Newspapers

BAADA YA KUFIWA NA MAMA WATOTO, DIDY ANG’OA KIFAA KINGINE

Siku moja baada ya mama watoto wa Diddy, ‘Kim Porte’ kufariki Dunia, rapa huyo ameonekana Los Angeles akiwa na mwanadada Cassie Ventura (32) ambaye waliachana Oktoba mwaka huu.

Camera ziliwanasa Ijumaa iliyopita, Novemba 16, 2018 wakitoka katika Taasisi ya Harakati huku Diddy akiwa amevaa sweta nyeusi na suruali nyekundu, Cassie alikuwa amevaa nguo zote nyeusi na waliingia kwenye gari moja aina ya Mercedes Benz na kuondoka pamoja.

Mahusiano ya Diddy na Cassie Ventura yalianza mwaka 2007 baada ya mwanadada huyo kukaa chini ya Label ya Bad Boy Record kwa muda wa miaka 7, na mahusiano yao waliyaweka hadharani mwaka 2012 ikiwa ni miaka 5 baada ya kuachana na aliyekuwa mama wa watoto wake ‘Kim’  ambaye ni marehemu kwa sasa hivi.

Kipigo Cha Stars Lethoto Mashabiki Wamvaa Kocha

Comments are closed.