BAADA YA KUFUNGIWA…DIAMOND, TANASHA KIMENUKA

DAR ES SALAAM: Kimenuka ile mbaya! Lile penzi shatashata lililotarajiwa kuzaa ndoa Februari 14, mwakani kati ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mtangazaji wa Kenya, Tanasha Donna ‘Zahara Zaire’, linadaiwa kupigwa na kimbunga cha hatari, Amani limeng’atwa sikio.

NI SIKU 25 TU

Kwa mujibu wa makabrasha yetu, penzi hilo hadi jana lilitimiza siku 25 pekee huku likiwa na wakosoaji kila kona ndani na nje ya Bongo.

NDOTO ZA NDOA ZAFIFIA

Amani linafahamu kwamba, tangu wawili hao wamekuwa pamoja na kutangaza kufunga ndoa, wapo watu waliokula kiapo kwamba ndoa hiyo haitafanikiwa hivyo kufifisha ndoto ya wawili hao kuoana.

WAFUTA PICHA

Kwa mujibu wa watu wa karibu na ‘kapo’ hiyo, ndugu, jamaa na marafiki, waliingiwa na ubaridi juzi baada ya kila mmoja kufuta picha za mwenzake kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram. Hata hivyo, baada ya zoezi hilo la kufutana picha, Tanasha aliibuka na kutetea uamuzi huo kuwa ulitokana na makubaliano yao kuwa kuanzia sasa walifanye penzi lao kuwa private (jambo lao binafsi) hivyo hawatakuwa wakijionesha mitandaoni.

WALIANZIA MWANZA

Hata hivyo, chanzo cha ndani kilishalitonya Amani mapema kuwa, wawili hao, wakiwa jijini Mwanza wikiendi iliyopita kwa ajili ya Tamasha la Wasafi Festival, kilinuka ile mbaya kwani walitibuana bila kufahamika chanzo ni nini ndipo likafuata zoezi la kufutana. “Mimi niwaambieni kitu, tayari kimenuka. Mimi niliwashuhudia kule Mwanza wakitibuana laivu, lakini sikujua ishu ilikuwa ni nini hadi niliposikia wamefutana picha kwenye Insta (Instagram).

WAKOSOAJI KIBAO

“Sioni dalili ya Mondi (Diamond) kumuoa Tanasha kwa sababu wakosoaji wamekuwa ni wengi. “Sikufichi, Diamond ameshajua kwamba alipotea njia ‘so’ anatafuta mahali pa kutokea. “Kibaya zaidi tayari ukweni kwa Diamond wameshajua kwamba hakuna ndoa hivyo wameanza kuchimba mkwara.

UKWENI WACHARUKA

“Wakenya mbalimbali ambao kwa muktadha huu ni wakwe wa Diamond walicharuka na kutishia kwamba, eti Mondi asipomuoa Tanasha, basi asikanyage Kenya.

Wakenya hao walisema kuwa, Diamond alishakuwa na Wema Isaac Sepetu na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kisha akaenda kwa Hamisa Mobeto japokuwa hakudumu naye hivyo sasa hivi yupo kwa Tanasha ambaye naye hawaamini kama kweli atamuoa. “Sasa Mondi ameshasikia hivyo vitisho kwa hiyo kimenuka ile mbaya. Kwa kifupi hawapo sawa sasa hivi,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa familia ya Diamond na kuongeza:

MAMA DANGOTE NAYE

“Hata mama Dangote (mama Diamond) anamkubali Tanasha kishingo upande anapoulizwa na vyombo vya habari, lakini ukweli ni kwamba hakumkubali. Kwanza wakati anatambulishwa kwa Tanasha, yeye mawazo yake yalikuwa kwa Kim Nana (video queen Lilian Kessy).”

Baada ya kujiri kwa sarakasi hizo, baadhi ya wachambuzi wa habari za mastaa Bongo walikuwa na mawazo tofauti;

“Diamond na Tanasha hawawezi kuoana na hata ikitokea hivyo hawatadumu.“Ndoa haitangazwi tu ghafla kama alivyofanya Diamond na kama utakumbuka, Paul Makonda (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam) alishasema kwamba Diamond siyo wa kuoa leo wala kesho kwani anahitaji kuongeza kwanza familia ya Wasafi iwe kubwa.

“Kingine Diamond siyo husband material (hana tabia za mwanaume aliye tayari kuoa) kama ambavyo Tanasha naye siyo wife material (hana tabia za kuwa mke). “Kama kweli Diamond alikuwa anataka mke wa kuoa, basi Zari alikuwa na sifa za mke, lakini siyo Tanasha. Huwezi kumfananisha huyo Tanasha na Zari hata kidogo linapokuja suala la wife material.

“Au huyo Tanasha atuambie tu kwamba amekuja kwa Diamond kuchuma mkwanja kisha anasepa, lakini wa kuolewa hawezi kuwa yeye,” alisema mchambuzi huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini na kuongeza: “Kwanza tayari Tanasha ameshajitengenezea taswira ya kutokubalika kwa Wabongo kitabia kuanzia mavazi hadi matumizi ya vileo.”

DIAMOND SIYO WA KUOA LEO

Ili kupata mzani wa habari hiyo, Amani lilimtafuta Diamond kujua msimamo wake kwa sasa, lakini simu yake ya kiganjani haikupokelewa na hata alipotumiwa ‘chatting’ kwenye WhatsApp hakujibu.

Lakini siku chache zilizopita kabla ya kuwa na Tanasha, mmoja wa waandishi wetu alimbana Diamond ambaye alijibu kwa kifupi:“Mimi siyo wa kuoa leo wala kesho.”

DIAMOND AONYWA MAMILIONI

Wakati huohuo, Diamond ameonywa juu ya video yake iliyosambaa ikimuonesha akihesabu mamilioni ya shilingi huku Tanasha akichukua video.

Kwa mujibu wa wadau waliozungumza na Amani walisema kuwa, yeye anaweza kuona kuwa ni ufahari, lakini ukweli ni kwamba anajihatarishia maisha. “Watu wengine wakiona vile wanaweza kudhani zile fedha anatembea nazo kwenye gari au amezihifadhi nyumbani hivyo akajikuta akivamiwa na hata kuuawa kwa jambo la kujitakia tu. “Anapaswa kuwa makini sana na asirudie tena jambo kama lile kwa usalama wake.”

TUJIKUMBUSHE

Kabla ya kutangaza ndoa na Tanasha, Diamond ambaye juzi alifungiwa kufanya shoo za ndani na nje, alishafanya hivyo kwa Zari ambaye alizaa naye watoto wawili, Wema, Jokate Mwegelo, Penniel Mungilwa na wengine, lakini ahadi hiyo haikutimia

Loading...

Toa comment