The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kufuta Tattoo ya Big Sean, Jhené Aiko Achora Hii (PICHA)

Baada ya aliyekuwa mpenzi wa Big Sean, Jhené Aiko Efuru Chilombo kuifuta Tattoo ya rapa huyo ili kupigilia msumari maneno yanayosemekana kwamba wawili hao hawapo pamoja, juzi Jumatano, Novemba 14, usiku alionekana katika viwanja Guggenheim jijini New York akiwa amechora tattoo nyingine mpya ambayo iliifunika ile ya Big Sean ilipokuwa mwanzo.

Tattoo hiyo mpya inamwonyesha Dragon akitema moto na nyingine ni ya Sola (kwa maana ya umeme wa jua).

 

Wawili hao hawajaonekana kwa muda pamoja na wala hakuna kati yao aliyethibitisha kwamba mahusiano yao yamevunjika.

 

Tweets mbili alizoandika Jhene Aiko baada ya Tattoo hizo kuonekana public zilikuwa zinaeleza kwamba ‘sanaa mpya’, ‘hakuna ugomvi’, ‘wote upendo’ na nyingine ikiendelea kusisitiza kwamba ni lazima aongeze tattoo.

ISIKUPITE: EXCLUSIVE INTERVIEW YA RAPA AY

 

Comments are closed.