The House of Favourite Newspapers

Breaking News: WAZIRI MKUU Ahairisha Bunge Hadi Mwakani – Video

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo amelihutubia Bunge wakati akiahirisha mkutano wa 13 wa bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

“Matukio ya ajali za bararani yamepungua kutoka ajali 9856 mwaka 2016, ajali 5578 mwaka 2017 na kufikia ajali 3209 katika kipindi cha Januari hadi Oktoba 2018. Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Oktoba 2018, Serikali imepeleka moja kwa moja kiasi cha shilingi 38.6 katika shule za Msingi na shilingi bilioni 44.6 zilipelekwa shule za Sekondari.

 

“Tangu kuanzishwa kwa elimu bure, uandikishwaji wa watoto wa awali na darasa la kwanza umeongezeka pia ufaulu wa mitihani ya darasa la saba umeongezeka kutoka wastani wa asilimia 70 mwaka 2016 hadi wastani wa 78 mwaka 2018.

 

“Shilingi Bilioni 9.2 zimeelekezwa katika kuimarisha miundombinu ya elimu kupitia program ya kuboresha elimu ya shule za msingi. Kupitia program ya lipa kulingana na matokeo katika elimu, jumla ya shilingi Bilioni 53.4 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shuoe za Msingi na Sekondari.

 

“Serikali iliunda tume ya kuchunguza chanzo cha ajali ya Kivuko cha MV Nyerere, tayari tumepokea taarifa hiyo na tunaendelea kuifanyia kazi. 

 

“Safari ya kuelekea AFCON iko nyeupe, sasa ni zamu yetu,” amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiahirisha mkutano wa Bunge jijini Dodoma leo.

VIDEO: MSIKIE MAJALIWA AKIZUNGUMZA

Comments are closed.