The House of Favourite Newspapers

BAADA YA KUITUNGUA YANGA, SASA KICHUYA AMEIFIKIA REKODI YA AMISS TAMBWE

0
Shiza Ramadhani Kichuya

Mchezaji wa Simba, Shiza Ramadhani Kichuya amefunga bao lake la tatu mfululizo dhidi ya Yanga kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom tangu asajiliwe na Simba msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Kichuya amefunga bao akiichezea Simba kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Yanga, Jumamosi hii. Kichuya alifunga bao hilo likiwa ni la kuongoza dakika ya 58 kipindi cha pili lakini halikudumu baada ya Obrey Chirwa kuisawazishia Yanga dakika ya 60.

Ikumbukwe kuwa Oktoba 1, 2016 Kichuya aliifunga Yanga kwa mara ya kwanza akiwa Simba bao lake likiwa ni la kusawazisha wakati timu hizo zilipotoka sare ya kufungana 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa.

Aidha, Februari 25, 2017 Kichuya aliifunga Yanga kwa mara ya pili mfululizo kwenye mechi za ligi Simba ilipopata ushindi wa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa.

Jumamosi ya Oktoba 28, 2017, Kichuya ameweka rekodi ya kuifunga Yanga kwa mara ya tatu mfululizo kwenye mechi za VPL mechi iliyochezwa uwanja wa Uhuru, Dar.

Mechi ambazo Kichuya ameifunga Yanga mfululizo

October 1, 2016 Simba 1-1 Yanga

February 25, 2017 Simba 2-1 Yanga

October 28, 2017 Yanga 1-1 Simba

Kichuya amefikia rekodi ya Amis Tambwe

Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe aliwahi kuifunga Simba mara tatu mfululizo tangu alipojiunga na Yanga baada ya kutemwa Simba.

Septemba 26, 2015, Tambwe aliifunga Simba kwa mara ya kwanza akiwa mchezaji wa Yanga wakati Yanga iliposhinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi.

Alifunga kwa mara ya pili kwenye ushindi mwingine wa Yanga 2-0 Simba Septemba 20, 2016 bao lake la tatu mfululizo dhidi ya Simba alilifunga October 1, 2017 wakati timu hizo zilipotoka sare ya kufungana 1-1.

Rekodi ya Amis Tambwe ya mabao matatu mfululizo vs Simba

September 26, 2015 Simba 0-2 Yanga

September 20, 2016 Yanga 2-0 Simba

October 1, 2017 Yanga 1-1 Simba

Leave A Reply