IKIWA ni muda mfupi baada ya akaunti za Instagram yenye jina la chadema_in_blood kuchapisha taarifa kwamba Mbunge wa Chalinze (CCM) ambaye pia ni mtoto wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete amekishutumu chama chake kwa kukubali kupokea wapinzania wanaohamia kwenye chama hicho, mbunge huyo ameibuka na kukanusha taarifa hizo.
Akifafanua kuhusu uzushi huo, Ridhiwani amesema hajawahi kusema wala kuandika maneno hayo, yanayolenga kukiambia Chama na Serikali yake, hivyo ujumbe huo upuuzwe mara moja.Aidha, amesema hatokuwa tayari kusema neno ambalo litapotosha kiapo chake kama Mwanasheria ninayeheshimu Haki na Usawa katika Binadamu.
Ujumbe huo ulisomeka hivi;
“Ridhiwani MTOTO WA KIKWETE AITOLEA UVIVU SERIKALI YA CCM NA CHAMA CHAKE.
“#Ashangaa serikali haijishitukii kumaliza fedha za wananchi kila kukicha kwenye chaguzi baada ya kuzitumia kwenye mahitaji ya wananchi ili kuwaletea maendeleo.
“Wakati wananchi hawana uhuru kupata habari za Bunge live kwa kisingizio cha kubana matumizi, leo gharama za kuendeshea, uchaguzi wa marudio Kinondoni peke yake unaigharimu serikali 1 bn Tsh.
“Hata kama wabunge na madiwani wa upinzani wanakipenda sana chama chetu na wanatamani sana kumuunga mkono Mhe Rais John Pombe Magufuli, hebu tusiwapokee, tuwaambie “Kaeni huko mtahamia 2020” ili fedha hizi tuzipeleke kwenye miradi ya maji, umeme, na elimu.
Ridhiwani Kikwete.”
Mimi
Ridhiwani Kikwete (Mb).”
Comments are closed.