The House of Favourite Newspapers

Baada Ya Kurejea Kambini… Mbrazili Simba Atenga Saa 120 Kumaliza Hesabu

0

BAADA ya kikosi chake kurejea kambini juzi Alhamisi, Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazil Roberto Olivieira ameweka wazi kuwa wameandaa programu ya mazoezi ya siku tano sawa na saa 120 kumaliza hesabu zao za msimu huu na kuanza rasmi maandalizi ya msimu ujao.

Simba wamesaliwa na michezo miwili ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Juni 6, mwaka huu kabla ya kumalizana na Coastal Union Juni 9, mwaka huu.

Kwenye msimamo, Simba wanakamata nafasi ya pili na pointi zao 67 walizokusanya kwenye michezo 28 waliyocheza, wakishinda mechi 20, sare saba na kupoteza mchezo mmoja.

Simba inaendelea na mazoezi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Simba MO Arena chini ya kocha huyo maarufu  kama Robertinho pamoja na wasaidizi wake.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Robertinho alisema: “Jambo zuri kwetu ni kuwa kikosi kimerejea kambini kwa ajili ya kumalizia maandalizi yetu ya michezo miwili iliyosalia na tumeandaa programu ya siku tano kumaliza kabisa hesabu za msimu huu.

“Baada ya michezo dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union ambayo itakuwa mwisho rasmi wa msimu kwetu tunatarajia kutoa mapumziko ya muda kwa wachezaji wote kabla ya kurejea kwa ajili ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘pre season’ ya msimu ujao.”

Stori na Joel Thomas

USIPIME MAYELE na MORRISON WAKIWASHA MAZOEZI ya MWISHO ya YANGA vs USM ALGIER…

Leave A Reply