The House of Favourite Newspapers

Baada Ya Nandy Atua Rasmi Kwa Mondi

0

GOOD news kwa mashabiki wa burudani ni kwamba, baada ya mtoto mzuri Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ kufanya kazi na mwanamuziki mkongwe wa Kongo, Antoine Mumba ‘Koffi Olomide’, taarifa mpya sasa ni rasmi mrembo huyo anakwenda kufanya kazi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, RISASI JUMAMOSI limedokezwa.

HAWAJAHI KUFANYA KAZI KABLA NA MONDI

Ikumbukwe, tangu Nandy atoke na kushika chati ya muziki wa Bongo Fleva kwa upande wa wasanii wa kike wanaofanya vizuri, amefanya kazi na wasanii wengi wazawa lakini hakuwahi kufanya na Diamond.

MINONG’ONO…

Kitendo cha kutofanya kazi na Diamond kimezua minong’ono mingi ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakieleza kuwa huenda wawili hao wana bifu la chinichini la kuwania utawala wa Bongo Fleva.

 

NANDY MKUBWA

Nandy amekuwa akifanya shoo kubwa zinazolingana kabisa hadhi yake na zile anazofanya Diamond kwenye viwanja mbalimbali vya mpira nchini jambo ambalo limekuwa likimpa ‘jeuri’ kwamba na yeye ni mkubwa kati ya wakubwa.“Yani kwa kweli natamani sana siku moja kuona Nandy anafanya kolabo na Diamond sijui itakuwaje maana wote wanajua,” mmoja wa wadau aliliambia RISASI JUMAMOSI wakati linakusanya maoni yake.

WADAU WANENA

Mbali na huyo, wadau wengi waliozungumza na RISASI JUMAMOSI kwa nyakati tofauti, walionesha wasiwasi wa kolabo hiyo kufanyika kutokana na uhasimu walionao.“Unajua Diamond ana utawala wake, Nandy naye ana nguvu yake hivyo nani unadhani atakuwa tayari kumueleza mwenziye kwamba wafanye ngoma ya pamoja?” alichangia Ema Masunga, mkazi wa Sinza Dar.

MTU WA NANDY ANENA

Risasi Jumamosi lilizungumza na mmoja wa watu wa karibu na Nandy ambaye alieleza jinsi ambavyo mrembo huyo anatamani kufanya kazi na Diamond lakini muda ulikuwa bado haujafika.“Kitambo tu sema ratiba zilikuwa zinaingiliana, Nandy anakuwa na mambo mengi hivyo kila akifikiria kufanya hivyo anajikuta yupo kwenye ziara ya muziki na mambo mengine ya bishara.“Unajua Nandy mbali na muziki, ana biashara nyingi sana ambazo zinamuingizia kipato na zote hizo zinamtegemea yeye hivyo lazima akose muda,” alisema mtu huyo.

 

AWASUBIRI WASAFI

Mtu huyo alizidi kumwaga ubuyu kwamba, kwa sasa Nandy yupo tayari kilichobaki ni uongozi wa Wasafi Classic Baby (WCB) kuafiki na kupanga siku ya kufanya.“Nandy anataka kufanya naye. Ameshafanya na Kiba, ameshafanya Koffi hivyo aliyebaki Kibongobongo ni Diamond tu.“Yeye atawaambia Wasafi dhumuni lake hivyo naamini kia kitu kitaenda sawa na watarekodi wimbo wa pamoja siku si nyingi,” aliweka nukta mtu huyo wa karibu.

HUYU HAPA NANDY

Baada ya kuachana na mtu huyo wa karibu na Nandy, RISASI JUMAMOSI lilimtafuta Nandy na kumuuliza kama kweli amepanga kufanya kazi na Diamond.“Yes, kwa nini tusifanye, tutafanya naye,” alijibu kwa kifupi Nandy.

 

TUJIKUMBUSHE

Nandy ambaye kwa sasa yupo nchini Uturuki kwa shughuli za kibiashara, kabla hajaondoka alikuwa ameachia wimbo wake na Koffi unaokwenda kwa jina la Leo Leo ambao mpaka sasa, tayari umeshatazamwa na watu Milioni 1.3 huko mjini YouTube.

 

Kuonesha kwamba bibie anajua, wimbo huo ambao ameuachia Februari 26, mwaka huu, unakamata nafasi ya pili kwa trending YouTube.

 

Nandy ndiye binti pekee ambaye kwa muda mrefu alikuwa ameushika utawala wa wasanii wa kike wanaofanya vizuri Bongo kabla ya Zuhura Othuman ‘Zuchu’ kuibuka na kumpa changamoto.

 

Hata hivyo licha ya kwamba Zuchu ameleta changamoto, bado Nandy amendelea kuwa mbele kwani yeye hayupo chini ya uongozi kama alivyo Zuchu chini ya WCB.Nandy yeye ni boss kama alivyo Diamond kwenye lebo yake. Mbali na kumiliki mjengo, Nandy anamiliki saluni kubwa inayouza bidhaa mbalimbali za wanawake ikiwemo magauni ya harusi.

STORI: MWANDISHI WETU

Leave A Reply