The House of Favourite Newspapers

Baada ya Pasaka Betika Mwendo Mdundo Kuwafikia Wadau

0

MAPEMA leo Jumatano, Aprili 15, 2020, timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea maeneo ya Temeke mwembeyanga na maeneo mengine ya  jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulinadi gazeti hilo.

Baadhi ya wazee wa kubeti wameendelea kulisifia kwa ujio wake huo kutokana na linavyoendelea kuwanufaisha katika kujipatia mkwanja kutokana na miongozo mizuri iliyopo ndani ya gazeti hilo inayowaongoza namna ya kubeti.

Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Leave A Reply