BABA DIAMOND KUKATWA MIGUU! – VIDEO

MUNGU amsaidie! Ndivyo walivyosikika, majirani wa baba wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa waliofika kumuona wakati waandishi wetu wakiwa wamewasili nyumbani kwa mzee huyo, Magomeni-Kagera jijini Dar kumjulia hali.  

 

Baada ya kujionea baba Dia­mond akiwa anasumbuliwa na tatizo la kansa ya ngozi, Ijumaa Wikienda lilimpigia simu dak­tari Godfrey Charle wa jijini Dar alipoelezwa kuhusu tatizo hilo, alisema kuna mambo ya kufanya ili kumnusuru kwani tofauti na hapo basi huenda akalazimika kukatwa miguu.

 

Awali, daktari huyo alianza kwa kuelezea hatua hiyo ya kansa kwa jinsi alivyoona picha na kueleza namna ambavyo inasam­baa katika mwili wa binadamu kutokana na maambukizi ya bakteria. “Kwa baba Diamond sambam­ba na kutibiwa kansa anatakiwa atibiwe pia maambukizi mbalim­bali yanayojitokeza kwani hayo ndiyo yanasababisha mgonjwa kukatwa mguu au kiungo chochote kilichoathirika na siyo kansa,” alisema daktari.

 

Daktari huyo baada ya kuzi­ona picha za namna ugonjwa huo ulivyoshambulia miguu ya baba Diamond (tazama picha ukurasa wa mbele), alisema upo uwezekano wa kupona kwa asilimia 50 lakini kwa jitihada za makusudi kutoka kwa familia au watu wanaomzunguka kum­saidia.

 

“Kwa kweli kwa hatua ile aliy­ofikia kupona kwake ni asilimia 50 tena kwa msaada wa ndugu yaani kama ndugu zake watam­saidia katika matibabu hivyo inategemea na msaada ataka­opata lakini vinginevyo asipopata msaada wa matibabu tena kwa haraka anaweza kukatwa miguu,” alisema dokta.

 

MAJIRANI WAMHURUMIA

Kutokana na hali aliyonayo, majirani mbalimbali waliokuwa wamefika kumuona baba Dia­mond, walionekana kumhurumia huku wengi wao wakionesha kutokuwa na la kufanya kwa kuwa hawana uwezo wa kifedha.

Jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdul, alisema wao kama majirani zaidi wanach­okifanya ni kumjulia hali mara kwa mara na kumpa pole lakini kimsingi wao hawana jinsi maana maisha yao ni ya kuungaunga.

 

“Kama unavyoona sisi mai­sha yetu yenyewe ndo haya hakuchi kunakucha tutafanya nini zaidi ya kumpa pole? Sana­sana mambo yakiwa freshi siku mojamoja tunamtoa hela kidogo lakini tatizo lake hili linahitaji hela nyingi,” alisema Abdul.

 

BABA DIAMOND

Akizungumza na Ijumaa Wik­ienda nyumbani kwake, baba Diamond alisema amepitia changamoto za muda mrefu kwa kusumbuliwa na miguu hiyo bila kupata matibabu hivyo ilifika wakati alikata tamaa ya maisha kabisa.

 

Alisema, amekuwa akihangai­ka katika hospitali mbalimbali na kupewa dawa tu za kutuliza maumivu lakini si hasa kutibu tatizo hilo la kansa kwani linahi­taji kuwa na fedha nyingi. “Kwa kweli miguu hii imen­isumbua kwa muda mrefu sana. Nimehangaika katika hospitali nyingi tu lakini kwa kweli nimeshindwa kujitibia kutokana na gharama kuwa kubwa,” alisema baba Diamond bila kuainisha gharama halisi zinazohitajika.

 

Alipoulizwa kama ame­shamwambia mwanaye amsai­die, baba Diamond hakutaka kumzungumzia lakini akasema anaamini kama ni tatizo hilo, Diamond atakuwa analifahamu vizuri maana lina muda mrefu. “Siwezi kumzungumzia sana lakini kikubwa mimi kwa sasa namshukuru Mungu kanikutani­sha na dada kutoka Uingereza anaitwa Zubeda Humphries ambaye amekuja na kuahidi kunisaidia ili niweze kutibiwa,” alisema baba Diamond.

 

Ijumaa Wikienda lilizun­gumza na dada huyo aliyejita­mbulisha kama dada wa hiyari wa Diamond ambaye alisema amekuwa akifuatilia tatizo la mzazi huyo kwa muda mrefu hivyo ameguswa kuja kumsaid­ia na atahakikisha anafanya kila linalowezekana ili aweze kumtibu sambamba pia na kumuunganisha na mwanaye Diamond.

 

“Diamond najua anawasaidia wengi hivyo naamini anaweza, mimi nitajitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu lakini pia nitajita­hidi kuwaunganisha na mwa­naye,” alisema dada huyo. Dada huyo pia aliwaomba viongozi wa serikali, taasisi mbalimbali ambazo zinaweza kuongeza nguvu katika kum­saidia basi waweze kujitolea. “Kutoa ni moyo na si utajiri, shime Watanzania tujitoe kum­saidia mzee huyu maana kwa kweli mimi nimemshuhudia kiukweli anaumwa,” alisema.

 

DIAMOND ANASEMAJE?

Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia ugonjwa huo wa baba yake hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kutopokelewa. Ijumaa Wikienda lilijaribu kuzungumza na mama Dia­mond, Sanura Kassim ‘Sandra’ alipokuwa msibani kwa msanii wa Hip Hop, Golden Mbunda ‘Godzilla’ lakini hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

 

HISTORIA INASEMAJE?

Diamond na mzazi wake huyo wamekuwa hawana uhusiano mzuri huku chanzo halisi cha uhusiano wao kuyumba kutoju­likana moja kwa moja. Hata hivyo, mara kadhaa mama Diamond amekuwa aki­wasiliana na mzazi mwenzake huyo lakini bado amekuwa aki­ishi kwenye mazingira magumu kwa kusumbuliwa na ugonjwa huo.

Loading...

Toa comment