SHOO YA MAHABA… MASTAA WATETEMA !

MJINI kuna vituko! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na mastaa mbalimbali wal­ivyotetema kwenye shoo ya Valentine iliyofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa King Solo­mon iliyopewa jina la Mahaba Full Chaji ambayo iliwafura­hisha na kukonga nyonyo za mashabiki waliohudhuria shoo hiyo.  

 

Burudani kibao zikiwemo za wanamuziki wa kizazi kipya, Ruby, Tonny Flavour, Barnabas Elius na wengineo zilitawala ambapo walikuwa wakipigiwa vyombo laivu na bendi ya Borabora Sound ambao nao waliongeza utamu wa shoo hiyo. Kutokana na burudani kuwa­konga nyoyo, mastaa walifanya vituko na vihoja kibao huku wengine wakikatiana nyonga hadharani na kusababisha shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki.

 

WOLPER AFUNIKA KUTE­TEMA

Msanii wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper aliwafunika mastaa wote kutetema kwa kukata nyonga kama zote huku akiwa amevaa kigauni kilichomuacha wazi sehemu kubwa ya maungo yake nyeti.

 

Kwenye shoo hiyo Wolper alimzimikia dogo ‘andagraundi’ aliyejulikana kwa jina la Maka Voice ambapo aliweka wazi jinsi anavyomzikia dogo huyo kwa ngoma yake aliyoitoa hivi karibuni ambayo hakuitaja jina ila aliimba kidogo. Akiwa kwenye kumpamba dogo huyo alimmwagia rundo la noti nyekundu. Tukio lingine lililowaacha hoi waliofurika ukumbini hapo ni kitendo cha mastaa kutengen­eza kapo lakini walipotakiwa kuweka wazi hilo kila mmoja alisema ni meneja wake.

Mkongwe wa filamu, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ ni kati ya kapo zilizonoga ukumbini hapo ikiwa ni baada ya mwanamama huyo kut­inga akiwa ameongozana na mwanaume flani mtanashati ambapo alipoulizwa kama ndiye shemeji alisema ni meneja wake ingawa mapozi yao yalizua utata hasa pale meneja huyo alipokuwa akim­bebea mpaka pochi.

 

Kapo nyingine iliyonoga ilikuwa ni ya Chegge na mwa­nadada aliyefahamika kwa jina moja la Beatrice ambapo waliingia wakiwa beneti lakini nao walipoulizwa Chegge al­isema huyo ni meneja ambaye anasimamia kazi zake pamoja na ‘andagraundi’, Maka Voice.

Wakati Chegge akiitolea nje kapo hiyo, mtangazaji wa Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ naye aliingia na mkaka mmoja mtanashati na kuten­geneza kapo matata ambapo walionekana wote kutinga mavazi meusi ambayo kwa kunogeshana zaidi wote walikuwa wakinywa kinywaji kinachofanana.

Kapu iliyowekwa wazi ni ya Ruby ambaye alimtambulisha baba kijacho wake kwa jina la Kusi Hozza ambao wao hawakuwa na cha kuficha, walikuwa ni mahaba full chaji.

Kwa upande wa Steven Mengere ‘Nyerere’ yeye aligeu­ka kuwa pedeshee kwani kutokana na kupagawishwa na burudani aliyokuwa akitoa jukwaani alimtuza Ruby noti nyekundu kibao pamoja na msanii chipukizi Maka Voice.

 

Ndani ya ukumbi huo burudani zilikuwa usipime kwani Barnaba alipopanda jukwaani alianza kuwachagiza mastaa hao kwa kuwaimbia nyimbo za miduara ambao kwa pamoja na mashabiki wengine walionekana kuban­juka ileile.

Loading...

Toa comment