The House of Favourite Newspapers

Baba P… Baba Pili… Baba Pilima!-16

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:
“Baba Pili… uwe basi baba Pilima moja kwa moja,” alisema mama Pilima akiwa na maana yake.
Baba Pili alikubali, akaitikia kwa kichwa huku akihema sana.
Ghafla, mama Pilima alimsukuma baba Pili, kule mpaka akaanguka chini!
SHUKA NAYO MWENYEWE…

“He! Vipi kwani?” aliuliza baba Pili akiwa ametumbua macho ya mshangao…
“Sitaki…unataka kuniteka kimapenzi baba Pili…unataka kuvunja ndoa yangu siyo?” alilalama mama Pili.

Kumbe mapigo ya baba Pili hata baba Pilima feki haoni ndani! Alifika mahali alitaka kupiga kelele kwa nguvu ndipo alipoamua kumsukumia mbali baba Pili ili atoe dukuduku lake hilo…

“Sasa jamani nitakutekaje wakati ni leo tu hatutaendelea tena?” alijieleza baba Pili huku akisimama kutoka sakafuni na kurudi kitandani. Alijiangalia kama ameumia…
“Nani kasema ni leo tu? Nitakuwa mjinga nikiacha mpira huu ukachezwa na wengine bila mimi kuwepo,” alisema mama Pilima kwa sauti ambayo ilionesha kutokuwa na utani hata kidogo.

Baba Pili wakati anapanda tena kitandani, mama Pilima alimvamia kwa kasi yote na kumlaza kisha mpira ukaendelea tena. Safari hii, kwa vile baba Pili alishajua kasi yake ni kubwa sana na imesifiwa, alizidisha kiwango hadi kufikia cha juu zaidi na zaidi.

Kazi kwa mama Pilima ikawa moja tu, kulalamika hata pale ambapo hakulalamishwa. Mwisho wa yote, wote walifika tamati ya mchezo kwa ushindi mkubwa na nderemo mbalimbali achilia mbali vifijo.

Sasa walikuwa wamelala, wanaangaliana kwa macho yaliyojaa aibu, hasa kwa mama Pilima…
“Baby,” alianza kusema mama Pilima akitumia jina la baby…
“Niambie mke wangu,” aliitika baba Pili.

Mama Pilima alijisikia vizuri sana kuitwa ‘mke wangu’ na baba Pilima. Mwanaume aliyetokea kuzidi kumpenda kwa siku hiyo kuliko siku nyingine yoyote ile, hasa kwa sababu ya kile alichofanyiwa kwenye sita kwa sita.
“Da! Basi tena,” alisema mama Pilima…
“Basi nini tena?”

“Itawezekana kwa mara moja tu jamani? Kwa mavitu haya?”
“Mimi nakusikiliza wewe tu,” alisema baba Pili huku akigeuka kumwangalia mama Pilima kwa macho yaliyojaa usingizi mzito lakini ni ule wa mahaba…
“Mh!” aliguna mama Pilima bila kucheka wala kuachia tabasamu.
***
Alichojua baba Pilima ni kwamba, kauli ya iwe mara moja tu ilikuwa palepale, hivyo alijiandaa kutoka kitandani ili akaoge…
“Unakwenda wapi baby?” aliuliza mama Pilima…
“Kuoga…”

“Kwani tunaondoka?”
“Ee…au?”
“Mh! Mimi sitaki…”
“Kwa hiyo tuendelee kuwepo?”
“Ikibidi.”

Ilibidi baba Pili arudi kitandani na kulala chali akiangalia juu. Mama Pilima akampelekea mkono mmoja, akamchezea kifuani, akashika kwenye ubavu na kuzitekenya mbavu, baba Pili akatetemeka lakini hakumshutumu.
Waligusanagusana wee, mwisho wakaanza raundi ya pili ambayo ilishika kasi ya kama dakika kumi tu, wote wakashangilia ushindi.

Sasa walikubali, baba Pili alikubali, mama Pilima alikubali zaidi. Ile wanamaliza tu kufurahia ushindi, simu ya mama Pilima iliita, baba Pili akiwa amelala mbele ya kitanda na mama Pilima akiwa mgongoni kwake, aliinuka na kuichungulia…
“Baby, leo baba Pilima anapiga sana…inakuaje? labda utoke hapo nje ukaongee naye,” alisema baba Pili…

“Mwache bwana…namjua huyo.”
“Unajua hata kama ni mimi mume wako siwezi kukubaliana na hali hii. Yaani nipige simu usipokee mpaka narudia tena? Haiwezekani mama Pilima,” alilalamika baba Pilima…

“Mimi namjua huyu…we achana naye bwana.”
Mama Pilima aliposema ‘namjua huyu’, baba Pilima hakujua kama mwenzake alimaanisha kumjua kwa maana si baba Pilima orijino, ni feki wakati baba Pili yeye alijua anamjua mumewe alivyo.
Simu ilipigwa hadi mara sita, mama Pilima hakupokea. Hilo lilimpa maswali kibao baba Pilima. Aliamini kwamba, kumbe kuna siku hata yeye atapiga simu halafu mwanamke huyo atakuwa anaingalia tu…

“Kumbe hata mimi utakuja kunifanyia hivi baby wangu,” alisema baba Pilima.
“Haitatokea baby. Unajua baby mtu ukitoka kufanya mambo kama haya halafu ukaongea kwa simu mtu anaweza kujua, maana kuhema kunakuwa kwingi ndiyo maana sitaki kupokea,” alisema mama Pilima, baba Pili akawa amemuelewa.

“Oke, nimekuelewa mama Pilima, lakini kuna jambo ambalo nataka kuzungumza na wewe kidogo,” alisema baba Pili…
Je, unajua ni jambo gani hilo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa, siku ya Ijumaa.

Leave A Reply