The House of Favourite Newspapers

Baba P… Baba Pili… Baba Pilima!-3

0

ILIPOISHIA..
“Sijawahi kusaliti na wala sipendi. Ingawa kama mwanamke naweza nikawa katika hali ya kujisikia kufanya hivyo lakini huwa najionya…”
Baba Pili alihema kwa nguvu na kumwangalia mwanamke huyo kisha akasema;
SOGEA NAYO…

“Unafikiri unaweza kukaa hivyo kwa kipindi gani?’ aliuliza baba Pili.
“Kwa kipindi kirefu lakini kumsaliti mume wangu naona ngumu sana,” alisema mama Pilima, kwa kumwangalia tu ungegundua kwamba aliamua kukaza kidogo, yaani kama gari, lilijifanya kutowaka ili litekenywe zaidi…

“Kwani kuna ubaya gani kama utatafuta kitu cha kukuridhisha hasa unapoona hauridhiki? Mama Pilima, tafuta haki yako, kufikishwa unapotaka kufika ndiyo kitu cha msingi kwenye mwili wako,” alisema baba Pili, sasa aliamua kumkazia macho mwanamke huyo, macho yenye kuelezea hisia zote za kimapenzi….
“Jamani mimi naogopa, atajua tu,” alisema mama Pilima….
“Atajuaje sasa? Au utamwambia?”
“Nimwambie! Sijitaki!”

“Sasa atajuaje? Hiyo itakuwa siri yako wewe na huyo mtu, yaani mtakuwa mkipiga shoo kimyakimya, hata majirani hawatajua,” alisema baba Pili….

Mama Pilima akanyamaza, alimwangalia baba Pili kwa macho ya kuita, yaliyolegea kama nyanya, alijitahidi kuyarembua kwa ishara ya kumwambia baba Pili, ‘sasa inakuwaje? Upo fiti nikupe chansi?’

Baba Pili alikuwa na mawazo yake, alichokifikiria kichwani mwake kilikuwa ni kumtega mwanamke huyo, kwanza ajue kama alikuwa mwepesi au laini.
Alishaanza kuchombeza, mifano mingi ya kumwambia amchukue mwanaume yeyote pasipo kujiweka wazi kwamba alitaka huyo mwanaume awe yeye.

“Kwa hiyo?” aliuliza baba Pili mara baada ya kupita ukimya kidogo.
“Ndiyo najifikiria hivyo mwenzio…”

“Jifikirie basi halafu chukua maamuzi, kila mwanamke anataka kuridhishwa bwana…” alisema baba Pili.

Waliendelea kuzungumza kwa muda huku taratibu wakiendelea kunywa pombe zao, walipomaliza, wakaagana tayari kwa kuondoka.
“Jamani! Kwa hiyo ndiyo basi hivyo?” aliuliza baba Pili.
“Kivipi tena?”

“Hata namba ya simu, sasa tutawasiliana vipi baada ya hapa?”
Mmh! Aya, subiri nikupe, andika..” alisema mama Pilima, hapohapo akampa namba ya simu baba Pili kisha kuondoka.

Njiani, baba Pili alichanganyikiwa, akawa hoi, mama Pilima alimuweka kwenye wakati mgumu, kwa kumwangalia tu, alionekana kuwa mwanamke mtundu sana kwenye sita kwa sita, kichwa chake kilimfikiria sana.

Kwa upande wa mama Pilima sasa, alipagawa, akasahau kama alikuwa mke wa mtu, mwanaume aliyekutana naye baa, alimuweka njia panda. Kiukweli hakutaka kabisa kumsaliti mumewe lakini kwa kile kilichokuwa kikiendelea, alishindwa kuvumilia.
“Kwa hiyo? Jitahidi tu, hatajua,” mama Pilima alisikia sauti ya baba Pili kichwani mwake.

“Nitajaribu…” alijikuta akiongea kwa sauti.
Wakati akifikiria hayo, ghafla simu yake ikatoa mlio wa kumjulisha kwamba kuna meseji ilikuwa imeingia, hapohapo akaifungua, alipoliona jina la baba Pili, akahisi mapigo yake ya moyo yakidunda kwa nguvu.

“Umefika?” iliuliza, harakaharaka akajibu…
“Ndiyo, nimejifungia chumbani tu, mpweke kweli…”
“Kwani baba Pilima hayupo?”

“Hayupo, amekwenda kuchukua mizigo yake ya ofisini, aliniambia kwamba kesho anasafiri, anakwenda Tanga kikazi, atakaa kwa wiki moja, hapa ndiyo nimechanganyikiwa, sijui itakuwaje,” aliandika mama Pilima.

Baba Pili hakutaka kuvumilia kuchati tu kwenye simu, alijiona anachelewa, hapohapo akamtwangia, alitaka kuzungumza naye zaidi.
“Umesemaje vile?” aliuliza baba Pili.
“Mume wangu anasafiri kesho…”
“Kweli?”

“Ndiyo! Sasa sijui itakuwaje…”
“Kwani huyo mtu umeshampata? Au mpaka umtafute?” aliuliza baba Pili.
“Bado…yaani sijui nitampata wapi! Kwanza najua leo hapa huyu mzee sijui kama atanipa haki yangu, na hata akinipa, sitaridhiki mie…” alisema mama Pilima kwa sauti ya kulalamika.

“Mmmh! Kwa hiyo itakuwaje? Au tuonane sehemu tulizungumzie hilo…”
“Lini?”
“Kesho.”
“Saa ngapi?”

“Muda wowote…yaani mimi nipo free, siendi popote pale, yaani popote pale sitokwenda,” alisema baba Pili, alisisitiza zaidi ili aonekane kweli alikuwa free.
“Basi tutapanga tuone inakuwaje…”
“Sawa..nimekuelewa, ninatamani sana nikuone, tena nimekumisi mno….” alisema baba Pili.

“Mmh! Yaani kipindi kifupi hiki umenimisi?”
“Ndiyo! Niliipenda sana kampani yako, umechangamka sana, unapendeza na unajua kuzungumza na mwanaume, naamini baba Pilima anafaidi sana dodo…” alisema baba Pili na mama Pilima akatoa kicheko kilichomwambia baba Pili, ‘na wewe unataka kula dodo? Basi karibu sisi twala…’

Itaendelea katika Gazeti la Ijumaa Wikienda.

Leave A Reply