The House of Favourite Newspapers

Baba P… Baba Pili … Baba Pilima!-4

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:
“Ndiyo! Niliipenda sana kampani yako, umechangamka sana, unapendeza na unajua kuzungumza na mwanaume, naamini baba Pilima anafaidi sana dodo…” alisema baba Pili na mama Pilima akatoa kicheko kidogo kilichomwambia baba Pili, na wewe unataka kula dodo? Basi karibu sisi twala…
ENDELEA SASA…

Mama Pilima alifika nyumbani akiwa mchangamfu hasa baada ya kukutana na baba Pili. Aliamini ameingiza kitu kipya katika maisha yake ya siku hiyo.
Aliweka simu juu ya meza, wifi yake anaitwa Sonia, alikuwa amekaa sebuleni. Mama Pili alikwenda chooni.

Baba Pili alipofika nje ya nyumba yake, aliamua kumpigia simu mama Pilima halafu ndiyo aingie ndani…

“Ngoja nimcheki huyu kwa simu kwanza ndiyo niingie, sijui kafika salama? Yaani bonge la demu ila hajijui tu…mtu kaumbwa utadhani kilitumika kiwanda…mimi yale macho yake du…halafu ana mwanya f’lani hivi…lakini saa zile alipoinuka kwenda toileti ndiyo nikamkubali.

“Ile ndiyo shepu bwana! Kabinuka halafu katikati pameingia…kwa kweli ni demu bomba kama nitampata lazima awe nyumba ndogo yangu…”
Simu ya mama Pilima iliita, wifi yake Sonia akainuka kuangalia anayepiga…
“Wifi…” aliita kwa sauti…

“Bee…”
“Kaka anapiga,” alisema Sonia baada ya kuona jina la baba Pili kwenye skrini.
Mama Pilima alitoka mbio akijua kweli ni mume wake…
“Mh!” aliguna kwanza alipoona jina la baba Pili…
“Eee…niambie…” alisema huku akienda chumbani…

“Ndiyo nimefika salama bwana…wewe je? Ahaaa! Sawasawa…”
Wakati mama Pilima anaendelea kuongea kwa simu huku akiingia chumbani, wifi yake alishangaa kumwona kaka yake baba Pilima anaingia…
”Khaa! Sasa wifi anaongea na nani? Mbona kaka kafika yeye bado anaongea chumbani?” alijiuliza…
“Shikamoo kaka…”

“Marhaba za hapa?”
“Njema…pole na kazi…”
“Nimepoa.”
“Wifi yako yuko wapi?”
“Nadhani chumbani.”

Baba Pili alinyoosha chumbani. Mkewe, alipoona mlango unasukumwa, alikata simu kwani alijua anayeingia bila hodi chumbani kwake ni mume wake tu.
Baada ya salamu, mama Pilima alitoka sebuleni na simu, akakaa kwenye sofa na kuanza kuchati…

“Nimepanda sauti yako baba Pili…la! mama Pili anafaidi sana hiyo sauti. Sijui unaitoaga kila mahali…!”
“Teh! Teh! Wewe acha maneno…si wewe mwenyewe unaogopa kuifaidi,” alijibu baba Pili…

“Wala siogopi, mwenzi sijawahi kusaliti. Ni hilo tu…kama ingetokea siku moja nimewahi kufanya hivyo hapo sawa, ningekuwa na uzoefu,” alijibu mama Pilima.
Walichati mengi sana, walichati mpaka sasa ikawa mama Pili anaandaa chakula huku akiwa anachati, yaani na simu mkononi. Akawa anaonekana akicheka, mara akitabasamu, mara akionekana kukazia macho simu…
***
Siku iliyofuata, mama Pilima alikwenda kwenye shughuli zake, alipomaliza jioni akiwa anarudi nyumbani kwake, alimkumbuka baba Pili…
“Si ajabu hata leo yuko pale pa jana…ngoja nimpigie,” alisema moyoni huku akiweka simu sikioni…

“Niambie mama Pilima,” alipokea baba Pili…
“Wapi?”
“Pana jana…”
“Ah! Nakuja…niagizie nusu rosti na ndizi moja…nakuja,” alisema mama Pilima…
“Sawa mama Pilima.”
Baada ya nusu saa, mama Pilima aliwasili. Alipofika, alimsogelea baba Pili, akambusu…
“Mmmwaaa…mmwaaa.”
“Da! Asante sana mama Pilima, nimejihisi nipo peponi leo. Nakupenda sana,” alisema baba Pili…

“Nakupenda pia baba Pili,” alijibu mama Pilima huku akivuta kiti na kukaa.
Walianza kuongea, wakaongea sana mambo yao. Ilifika mahali baba Pili akaanza kukumbushia ya jana yake…

“Vipi mama Pilima, bado una msimamo uleule?” aliuliza baba Pili…
“Da! Baba Pili unajua nikwambie kutoka moyoni kwamba mimi sijawahi kusaliti hata siku hii…moja! Sasa leo hii nikisema nijaribu huoni kuwa, siku ikitokea umenimwaga nitaanza kutafuta wanaume wengine, mwisho wake nitakuwa malaya…”
“Mh! Mimi mpango wangu ni kukufanya uwe nyumba ndogo yangu,” alisema baba Pili, mama Pilima akacheka sana…

“Sasa niwe nyumba ndogo yako baba Pili si utakuwa unapata shida? Mimi najua nyumba ndogo lazima iwe free…ukitaka kwenda unakwenda muda wowote ule.”

“Hapana si lazima…unaweza kuwa mke wa mtu halafu bado ukawa nyumba ndogo yangu,” alifafanua baba Pili akionekana yuko siriasi kabisa na maneno yake…

Je, nini kiliendelea? Fuatilia katika Gazeti la Ijumaa siku ya Ijumaa.

Leave A Reply