The House of Favourite Newspapers

Baba P… Baba Pili… Baba Pilima!-5

1

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA:

“Sasa niwe nyumba ndogo yako baba Pili si utakuwa unapata shida? Mimi najua nyumba ndogo lazima iwe free…ukitaka kwenda unakwenda muda wowote ule.”
“Hapana si lazima…unaweza kuwa mke wa mtu halafu bado ukawa nyumba ndogo yangu,” alifafanua baba Pili akionekana yuko siriasi kabisa na maneno yake…
JIACHIE MWENYEWE…

“Mh! Mimi nadhani au napendekeza tuendelee kuwa kama hivi…marafiki wakubwa lakini wa siri…mume wangu baba Pilima asijue wala mke wako mama Pili asijue…tutafurahi sana,” alisema mama Pilima huku akionekana kuachia tabasamu la mbali sana.

Hapo bia zilikuwa zikimiminika mezani. Ilifika wakati walianza vituko wakiwa wamekaa, mama Pilima alimkanyaga baba Pili, naye baba Pili akamkanyaga mama Pilima, wakaangaliana, wakachekea ndani kwa ndani, mama Pilima akamsogelea baba Pili, akatoa ulimi kuelekea kwake, baba Pili akaudaka…

Waligugumia, mihemko ilitawala, baba Pili akapeleka mkono kwenye kifua cha mama Pilima maana eneo hilo la baa walilokaa lilikuwa halina watu hata kidogo.

Kumbe mkono wa baba Pili kwenye kifua cha mama Pilima ulifanikiwa kushika nido za mwanamke huyo, akashtuka kwa maumivu ya mahaba. Ilimpa picha baba Pili kwamba, udhaifu wa mapenzi wa mama Pilima upo kifuani, akautoa mkono maana alijua kweli si mahali pake, pale ni baa.

Mama Pilima kuona amegundulika udhaifu wake, naye akawa anautafuta udhaifu wa mwanaume huyo, akapeleka mkono kifuani na kuchezea ‘bustani’ ya hapo lakini baba Pilima wala!

Akautoa mkono hapo, akamshika shingoni, wala! Akaupeleka mkono mgongoni, wala! Akaushusha, baba Pilima akalainika sana lakini hakushtuka kama alivyoshtuka yeye mama Pilima alipoguswa nido.

Mama Pilima akajua kumbe udhaifu wa mwanaume huyo upo huko, akatoka na kushika glasi ya bia lakini hakuipeleka kinywani, aliendelea kubakiza ulimi wake ndani ya kinywa cha baba Pili huku akisikika kwa sauti ya…
“Mmm…mmm…mmm!”

Waliachana kwenye denda baada ya miguu ya mhudumu kutembea kuelekea walipokaa…
“Niongeze?” aliuliza mhudumu.

Mama Pilima alishika chupa ya bia ya baba Pili, akaitingisha, akaiweka chini, akashika ya kwake, akaitingisha, akaiweka chini…
“Ongeza kwa bili yangu tafadhali,” alisema.

Mhudumu alipoondoka tu, mama Pilima akaanza, akapeleka mkono kulekule alikogundua ndiko kwenye udhaifu wa baba Pili. Safari hii akaonesha hana mpango wa kuutoa haraka.

Huku akiangalia upande atakaotokea mhudumu, mama Pilima alifanya yake huku baba Pili akisinzia kwa starehe. Na vile alikuwa tayari yuko vizuri, looo!
Hali ya baba Pili ilimnasa hata mama Pilima mwenyewe aliyekuwa akisababisha. Naye akawa anaguna, anagugumia, anahemuka na anasinzia.

Kuna wakati wote walijikuta wamesinzia lakini mkono wa mama Pilima ukiwa bado kazini. Wakashtuka mhudumu alipoweka chupa za bia mezani kwa kuliza puu!
Mama Pilima ili asionekane alikuwa anafanya jambo baya, aliendelea kuuacha mkono kule…

“Fungua chapuchapu!” alisema.
Mhudumu alifungua, lakini alijua nini kilikuwa kinaendelea kwenye meza ile.
Baada ya mhudumu kuondoka, mama Pilima akakazana, baba Pili akahisi anaonewa, naye akarudia kwenye udhaifu wa mama Pilima. Sasa wakakaa kwa kuangaliana, mama Pilima kule, baba Pili pale. Walisisimka, wakashindwa kuvumilia hivyo, waliamua kuacha kwa mama Pilima kutoa kauli…

“Basi bwana! Tunakwenda kubaya,” alisema kwa sauti ya kukatakata ikitoka nje kwa njia ya puani.

Mama Pilima alivuta pumzi kwa nguvu, akazishusha huku akimwangalia baba Pili bila kusema lolote.

Baada ya hapo, waliendelea kunywa bila kusemezana, ilionekana kila mmoja alikuwa akiwaza yake moyoni kuhusu walikofikia awali.

Muda wa kufunga baa ulifika, mhudumu alikwenda kuchukua pesa yake, akalipwa! Wawili hao waliondoka huku wakiyumbayumba, wakashikana mikono ili kusaidiana kutembea.

Mama Pilima hakuwa na usafiri, baba Pili alikuwa nao, akampakia mwanamke huyo katika hali ya uleviulevi…

Baba Pili yeye ni mzima akiwa barabarani, aliendesha gari hadi Magomeni Kagera, akamshtua mama Pilima…

“Oho! Twende hadi mbele, kata kushoto, mbele utasimama. Baba Pili akafanya hivyo.
Walifika eneo la kusimama, gari likasimamishwa…
“Sasa?” aliuliza mama Pilima…
“Umefika bado?” aliuliza baba Pili…

“Nikishuka natembea kidogo mpaka kule mbele, lakini hapa panatosha,” alisema mama Pilima, wakaangaliana kwa muda mle ndani ya gari.

Wakasogeleana kama watu waliokuwa wakisikiliza maelekezo ya pamoja. Wakakutanisha midomo, wakaifungua, wakaanza kucheza na denda. Wakawa wanaguna ndani kwa ndani mpaka baba Pili akazima gari…

“Sogeza gari kwa pale mbele basi,” alisema mama Pilima kwa sauti ya kuchoka sana.
Baba Pilima akawasha tena gari, akalisogeza mpaka eneo aliloambiwa na mama Pilima…
“Hapa?”

“Yes! Hakuna mtu anayepita eneo hili muda huu,” alisema mama Pilima hali iliyomfanya baba Pili aamini kwamba huenda wanakwenda kutimiza ndoto yake…
“Egemea kiti,” alisema mama Pilima…

Je, unajua nini kilitokea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, siku ya Jumatatu.

1 Comment
  1. Godwin malila says

    Baba p nimeikubali

Leave A Reply